Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
1 6 /
M U N G U B A B A
hupendelea kuhoji kama ni kweli kuna Mungu au la, yaani, kama ni kweli yuko Mungu mbinguni, Biblia haijihusishi kwa namna yoyote na mjadala wa jinsi hiyo. Kinyume chake, ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu kwa sababu wamepinga kile kinachojulikana kumhusu Mungu. Sifa za Mungu zisizoonekana , zile sifa na tabia ambazo wanadamu hawawezi kuziona kwa macho ya nyama, uweza wake wa milele na asili ya kiungu, kulingana na Paulo zinafahamika wazi tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Vitu ambavyo Mungu wetu mkuu ameviumba, jua na mwezi, nyota katika utukufu wake, na dunia katika fahari yake, vyote kwa pamoja vinaonyesha kwamba Mungu sio tu ni halisi, lakini pia ni mwenye uweza wote na utukufu. Mtu anawezaje kutazama ndege warukao kwa mbawa, kusikia mtoto mchanga akilia, kuona kundi la mifugo wakilishwa kwenye uwanda wa kijani unaovutia chini ya anga angavu linalong’aa, na kusema kwamba hakuna Mungu? Mtu anawezaje kupigwa na upepo mkali usoni wakati wa usiku katika msimu wa baridi, au kuona mwezi ukining’inia usiku kwa umaridadi wote katika msimu wa masika, au kuona farasi akikunjua mguu wake na kupiga hatua kamili na kuamini kabisa kwamba hakuna ufahamu wa hali ya juu nyuma ya uzuri uliotukuka wa dunia? Mpendwa rafiki, hoja yenye kushawishi zaidi kuhusu uwepo wa Mungu si ya kifundisho, ni yale yanayoonekana. Zaburi 19:1-3 - “Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, Na anga laitangaza kazi ya mikono yake. 2 Mchana husemezana na mchana, Usiku hutolea usiku maarifa. 3 Hakuna lugha wala maneno, Sauti yao haisikilikani.” Neno hili dhahiri la Maandiko linasisimua: mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, na anga laitangaza kazi ya mikono yake. Yaliyozungumzwa kuhusu uumbaji wa Mungu yamejitosheleza kiasi kwamba mtu yeyote mwenye akili timamu lazima akubali kwamba nyuma ya utukufu huu kuna uwepowa kiungu. Tatizo la wasioamini katika Mungu na wenye mashaka kuhusu Mungu si kutokuwepo kwa ushahidi wa kutosha, bali ni kwamba mioyo yao wenyewe ni migumu. Kuna uthibitisho wa kumtosha mtu kutubu; mwenye shaka hana udhuru wa kutokumjia Masihi. Baada ya kutamka na/au kuimba Kanuni ya Imani ya Nikea (katika kiambatisho), sali sala ifuatayo: Ee Mungu, ukuu wako unaijaza dunia na ulimwengu wote, lakini ulimwengu wenyewe hauwezi kukutosha, sembuse dunia, achilia mbali ulimwengu wa mawazo yangu. ~ Yves Raguin, SJ. Appleton, George, mhariri. The Oxford Book of Prayer. Oxford; New York: Oxford University Press, 1988. uk. 4
1
Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi
Made with FlippingBook - Online catalogs