Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
/ 1 7 1
M U N G U B A B A
K I A M B A T I S H O C H A 1 4 Majina ya Mwenyezi Mungu Mch. Dkt. Don L. Davis
I. Majina ya Mungu
A. Elohim 1. Elohim ni wingi wa Kiebrania uliotumika zaidi ya mara 2000 katika Agano la Kale, kwa kawaida huitwa “wingi wa ukuu” wa jina la jumla la Mungu. 2. Linatokana na El, ambalo maana ya mzizi wake ni “kuwa na nguvu” (rej. Mwa. 17:1; 28:3; 35:11; Yos. 3:10) au “kuwa mkuu.” (rej. Frank M. Cross, “El,” katika Theological Dictionary of the Old Testament, 6 vols., iliyofanyiwa mapitio, iliyohaririwa na G. Johannes Botterweck na Helmer Ringgren (Grand Rapids: Eerdmans, 1977, 1:244). 3. Elohim kwa kawaida hutafsiriwa kama “Mungu” katika tafsiri za Kiingereza. 4. Jina hili linasisitiza sifa ya Mungu ya kuwa juu ya vyote (rej. kwamba Mungu yu juu ya wengine wote waitwao Mungu). Elohim ni wingi wa El ; maneno haya yanaonekana kutumika kwa kubadilishana (rej. Kut. 34:14; Zab. 18:31; Kum. 32:17, 21). 5. Katika baadhi ya maandiko (kama vile Isa. 31:3) El inaweza kumaanisha “uwezo na nguvu za Mungu na kwa upande mwingine maadui wa kibinadamu kutokuwa na uwezo wa kujilinda na kujihami mbele zake” (rej. Hos. 11:9). (Rej. 34. Helmer Ringgren, “Elohim,” katika Theological Dictionary of the Old Testament, 1:273-74). B. Adonai 1. Neno Adonai (Kiebr. Adhon or Adhonay ) katika mzizi wake linamaanisha “bwana” au “mkuu” na kwa kawaida hutafsiriwa “Bwana” katika Biblia za Kingereza. 2. Linatokea mara 449 katika Agano la Kale na mara 315 likitumiwa pamoja na Yehova. Adhon linasisitiza uhusiano wa mtumishi na bwana (rej. Mwa. 24:9) na kuashiria mamlaka ya Mungu kama Bwana, yaani, Mmoja atawalaye kwa mamlaka kamili (rej. Zab. 8:1; Hos. 12:14).
Made with FlippingBook - Online catalogs