Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook

1 7 6 /

M U N G U B A B A

Maono na Mbinu za Kitheolojia (muendelezo)

C. Hoja ya Kiteleolojia – (fizikia ya kiteleolojia) 1. Telos = mwisho

2. Mambo katika uzoefu wetu yanaonekana kuwa na malengo zaidi ya kuwepo kwake. Kusudi katika asili, linamaanisha uko ufahamu wa hali ya juu. 3. Hati muhimu: kusudi halitokei bila Mwenye kuliweka. D. Hoja ya kimaadili – Watu wa tamaduni na imani mbalimbli hutambua maadili na wajibu fulani wa kimsingi. 1. Maadili haya ya jumla hayawezi kupunguzwa na kufanywa kanuni tu. 2. Haya hayatoki kwenye ulimwengu unaoonekana. 3. Kwa hiyo, tunaweza kutoa hoja ya uwepo wa mmoja mwenye maadili makuu, kama chanzo cha maadili yote na kama ambaye viumbe vyote vya kimaadili huwajibika kwake.

II. Kweli Kuhusu Theolojia ya Asili

A. Iliyopo zaidi katika Theolojia ya Kikatoliki

B. Theolojia ya Ki-Kalvini: inaamini katika ufunuo wa jumla wa Mungu katika asili na utawala. 1. Inauzungumzia “uungu” au “hisia ya kuwepo kwa Mungu” ambayo ilikuwa ‘chanzo cha dini.’ 2. Kupata maarifa ya hakika ya Mungu ni lazima tuligeukie Neno la Mungu katika Maandiko.

C. Karl Barth: alikataa theolojia ya asili katika ujumla wake kwa misingi ya kwamba Mungu amejifunua katika Neno lake, na haina maana kuangalia mahali pengine.

Made with FlippingBook - Online catalogs