Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook

/ 1 8 3

M U N G U B A B A

K I A M B A T I S H O C H A 1 9 Kuangazia Mifumo Tofauti ya Fikra Mfumo wa Fikra uliounganishwa na Mfumo wa Fikra Uliogawanyika Dkt. Don L. Davis

Mtazamo na Mfumo wa Maisha uliogawanyika

Mfumo wa Maisha na Mawazo yaliyojumuishwa

Huona mambo kimsingi kuhusiana na mahitaji ya mtu mwenyewe Huona kitu kingine zaidi ya Mungu kama sehemu mbadala ya rejea na uratibu wa maana na ukweli. Hutafuta baraka za Mungu kwa lengo la uboreshaji wa mambo binafsi ya mtu mwenyewe. Huelewa madhumuni ya maisha kuwa ni kupata kiwango kikubwa zaidi iwezekanavyo cha utoshelevu na uboreshaji wa mambo binafsi. Huhusiana na wengine kwa msingi pekee wa athari (faida) na nafasi (fursa) walizonazo katika masuala binafsi ya mhusika.

Huona vitu vyote katika muono wa umoja na jumuishi

Humwona Mungu katika Kristo kama sehemu kuu ya rejea na uratibu wa kutoa maana yote na ukweli. Huoanisha malengo binafsi na mpango mkuu wa Mungu na makusudi yake. Huelewa kusudi la maisha kuwa ni kutoa mchango mkubwa iwezekanavyo kwa kusudi la Mungu ulimwenguni. Hujihusisha kwa kina na watu wote na masuala yote kama sehemu muhimu ya mpango mkuu wa Mungu kwa utukufu wake (Mungu) mwenyewe. Hufafanua theolojia kama kutafuta kufahamu miundo na mipango mikuu ya Mungu kwa ajili yake mwenyewe katika Yesu Kristo. Hutendea kazi Neno kama matokeo ya kuelewa kile ambacho Mungu anajifanyia Mwenyewe katika ulimwengu. Hujikita katika mtindo wa usanisi (kutambua muunganisho na umoja wa vitu vyote). Hutafuta kuelewa ufunuo wa kibiblia kimsingi katika mtazamo wa mpango wa Mungu katika upana na ukamilifu wake (“mpango wa Mungu kwa vizazi”). Hufanya maamuzi akiongozwa na nia ya kujitolea kushiriki kama mtenda kazi pamoja na Mungu katika maono mapana ya Ufalme (“Mungu anafanya kazi duniani”). Hujiunganisha na kujifungamanisha kwenye maono na mpango wa Mungu kama msingi na kiini cha utendaji kazi Huona utume na huduma kama udhihirisho wa sasa wa kivitendo wa utambulisho wa mtu kulingana na maono mapana ya Mungu. Huhusianisha maarifa, fursa, na shughuli na maono na kusudi moja lililounganishwa. Maisha yote yanaendeshwa kuzunguka mada moja: ufunuo wa Mungu katika Yesu wa Nazareti.

Hufafanua theolojia kama kutafuta kueleza mtazamo wa mtu fulani juu ya wazo au dhana fulani ya kidini.

Hutendea kazi Neno katika msingi wa kutafuta majibu sahihi kwa masuala na hali fulani.

Hujikita katika mtindo wa uchanganuzi (kutambua michakato na muundo wa vitu). Hutafuta kuelewa ufunuo wa kibiblia kimsingi katika mtazamo wa maisha binafsi ya mtu (“mpango wa Mungu kwa maisha yangu”). Hutawaliwa na fadhaa kubwa ili kuhakikisha usalama wa mtu mwenyewe na umuhimu katika juhudi alizochagua (“Mpango wangu kwa maisha binafsi”). Hujiendesha kwa minajili ya kukidhi mahitaji binafsi na kuyafanya malengo binafsi kuwa misngi na kiini cha utendaji kazi. Huona utume na utumishi kama fursa ya kuonyesha vipawa na mzigo wa mtu binafsi, ili kuleta utoshelevu na usalama binafsi. Huhusianisha maarifa, fursa, na shughuli na malengo ya kujiboresha na kutafuta utoshelevu binafsi. Maisha yote yanaongozwa kuzunguka utambulisho binafsi na mahitaji ya mtu binafsi.

Made with FlippingBook - Online catalogs