Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook

/ 1 8 5

M U N G U B A B A

Kuangazia Mifumo Tofauti ya Fikra (muendelezo)

katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili. 10 Na ninyi mmetimilika katika yeye aliye kichwa cha enzi yote na mamlaka. 1 Yohana 5:11-12 - Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe. 12 Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima. Zaburi 16:5 - Bwana ndiye fungu la posho langu, Na la kikombe changu; Wewe unaishika kura yangu. Zaburi 16:11 - Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako ziko furaha tele; Na katika mkono wako wa kuume Mna mema ya milele. Zaburi 17:15 - Bali mimi nikutazame uso wako katika haki, Niamkapo nishibishwe kwa sura yako. Waefeso 1:9-10 - akiisha kutujulisha siri ya mapenzi yake, sawasawa na uradhi wake, alioukusudia katika yeye huyo. 10 Yaani, kuleta madaraka ya wakati mkamilifu atavijumlisha vitu vyote katika Kristo, vitu vya mbinguni na vitu vya duniani pia. Naam, katika yeye huyo. Yohana 15:5 - Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote. Zaburi 42:1 - Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji. Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu. Habakuki 3:17-18 - Maana mtini hautachanua maua, Wala mizabibuni hamtakuwa na matunda; Taabu ya mzeituni itakuwa bure, Na mashamba hayatatoa chakula; Zizini hamtakuwa na kundi, Wala vibandani hamtakuwa na kundi la ng’ombe; 18 Walakini nitamfurahia Bwana Nitamshangilia Mungu wa wokovu wangu. Mathayo 10:37 - Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili. Zaburi 37:4 - Nawe utajifurahisha kwa Bwana, Naye atakupa haja za moyo wako. Zaburi 63:3 - Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai; Midomo yangu itakusifu. Zaburi 89:6 - Maana ni nani katika mbingu awezaye kulinganishwa na Bwana? Ni nani afananaye na Bwana miongoni mwa malaika?

Made with FlippingBook - Online catalogs