Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook

1 9 2 /

M U N G U B A B A

K I A M B A T I S H O C H A 2 4 Nadharia za Uvuvio Mch. Terry G. Cornett

Nadharia za Uvuvio

Maelezo

Pingamizi zinazowezekana kuwepo

Mwandishi wa kibinadamu ni kifaa mikononi mwa Mungu kisichokuwa na athari. Mwandishi anaandika tu kila Neno kama Mungu anavyoliongea. Uandishi huu wa moja kwa moja ndio unaozuia andiko kuwa na makosa ya kibinadamu.

Vitabu vya Maandiko vinaonyesha mpangilio tofauti wa uandishi, msamiati, na namna ya kuelezewa ambayo inatofautiana kutoka kwa mwandishi mmoja na mwingine. Nadharia hii haionyeshi kuelezea kwanini Mungu alitumia waandishi wa kibinadamu badala ya kutupa Neno lililoandikwa moja kwa moja kutoka kwake mwenyewe. Biblia inaonyesha kwamba Maandiko yalitoka kwa Mungu, kupitia waandishi wa kibinadamu (2 Pet. 1.20-21). Maandiko yanaonyesha kwamba waandishi wa kibinadamu walionyesha Neno halisi la Mungu (hasa maandiko yanayoonyesha maneno “asema Bwana”; Rum. 3.2.) Waandishi wa Biblia kamwe hawajawahi kuonyesha kwamba Maandiko fulani yamevuviwa zaidi au kushughulika na aina moja tu ya Maandiko kama ndio iliyovuviwa katika matumizi yao. Yesu anaongea kuhusu ufunuo wote wa Maandiko mpaka siku ya kwake kwamba ni Neno toka kwa Mungu lisilobadilika (Mt. 5.17-18; Yohana 3.34-35). Inaonekana kama vile haiwezekani kwamba vipengele vya kibinadamu ambavyo vina mwisho wa matumizi yake na vyenye kujishikiza kwenye utamaduni fulani tu vingeweza kuelezewa kama Neno la Mungu lisilobadilika

Nadharia ya Uvuvio wa Kiimla

Nadharia ya Uvuvio wa Kihisia au Wa Asili

Watu wenye karama na maono ya kipekee ya kiroho walikuwa wanachaguliwa na Mungu kuandika Biblia

Roho Mtakatifu aliongeza kimo cha uwezo wa kawaida wa uelewa wa waandishi wa kibinadamu ili kwamba wawe na maarifa ya kipekee kwenye kweli ya kiroho.

Nadharia ya Kuangaziwa

kwa maandiko (Illumination)

Sehemu fulani za Biblia zimevuviwa zaidi kuliko nyingine. Wakati fulani sehemu hii huwa inatumika kujadili kwamba sehemu za Biblia zinazohusika na mafundisho ya msingi na kweli za kimaadili zimevuviwa zaidi, wakati sehemu za Biblia zinazohusika na historia, uchumi, utamaduni n.k zimevuviwa kidogo au hazijavuviwa kabisa. Viashiria vyote vya kimungu na kibinadamu vipo katika uzalishaji wa Maandiko. Kifungu chote cha Maandiko, pamoja na maneno yote, ni zao la ufahamu wa Mungu ulioelezewa kwa namna na hali ya kibinadamu, kupitia waandishi wa kibinadamu ambao aliwafahamu tangu Mwanzo (Yer. 1.5) na kuwachagua kwa ajili ya kazi yake.

Nadharia ya Viwango vya

uvuvio (au Uvuvio wa sehemu)

Nadharia ya Uvuvio wa

neno kwa neno – Uvuvio Kamili

Made with FlippingBook - Online catalogs