Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
2 2 2 /
M U N G U B A B A
Kutoa Utukufu kwa Mungu (muendelezo)
3. Usimwabudu mungu wa michezo. 4. Usitoe dhabihu kwa mungu wa ndoa na familia. 5. Usitafute kumtukuza mungu wa kabila na nchi.
6. Usimwabudu mungu wa kazi. 7. Usimsujudie mungu wa mali. 8. Mungu wa dini. 9. Vielelezo. a. Sisi kama jamii tuna ukereketwa na na mihemko kwa ajili ya Michael Jordan na Michael Jackson kuliko Bwana Yesu. b. Watu wamejitoa zaidi kwa nchi, rangi, utamaduni, na ukoo kuliko Kristo. c. Alichokisema John Lennon kuhusu bendi ya muziki ya the Beatles. C. Tatu, tunaweza kumnyang’anya Mungu utukufu unaomstahili kwa kutopendezwa na sifa zake —kutojali kwa njia moja au nyingine. 1. Tunaweza kutotilia maanani na hata kutokujali kuhusu kile tunachompa Mungu , Mal. 1:7. 2. Tunaweza kuona kwamba kumpa Mungu utukufu ni jambo la kujidhalilisha (hili ndilo kosa na tatizo la vijana wengi ambao huhisi kama wanalazimishwa kumwamini Mungu kwa sababu ya imani ya wazazi wao), Mal. 1:7. Je, unadhani ni kazi gani kuu ya mmoja wa wajaribu wa kipepo kwa wanadamu, ni nini wanachotaka kufanya zaidi? C.S. Lewis, mwandishi wa The Screwtape Letters , anasema kwamba ni kukufanya usijali mambo ya Mungu. Katika kitabu hiki shetani anamshauri mpwa wake, Mchungu, juu ya hila na mbinu za kuwajaribu watu. ‘Lengo,’ anasema, ‘Si uovu bali ni kutojali.’ Shetani anamwonya mpwa wake kutufanya, sisi walengwa na wagonjwa wake, kuwa na amani na utulivu kwa vyovyote vile. ‘Kama atapaswa kulifikiria jambo lolote lenye umuhimu, mtie moyo aifikirie mipango mingine midogo’; anamwambia ‘usijali, hilo linatosha kuwasababishia kuvimbiwa.’ Kisha shetani anamshauri tena mpwa wake kwa
Made with FlippingBook - Online catalogs