Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
4 0 /
M U N G U B A B A
Moyo hasa wa somo hili ni kwamba Mungu yuko na anatenda kazi vile vile hana kikomo na yuko juu zaidi ya uumbaji wote. Yeye hujifunua kwa watu wote kupitia uumbaji wake mtukufu, na bado, yeye binafsi hufunua moyo na nafsi yake kwa wote wanaotubu na kumwamini Yesu Masihi. Mtafute Bwana kwa ajili ya nguvu zake na hekima ya kuyaishi kwa uaminifu yale unayoyajua na kuamini kuhusu Mungu, na uombe msaada wake katika kukusaidia kuwasilisha kwa uwazi na ujasiri kweli kuhusu sifa tukufu za Mungu na nafsi yake. Omba usaidizi kutoka kwa viongozi na mkufunzi wako katika eneo lolote ambalo Mungu anaweza kuwa anazungumza nawe, na omba ujazo wa Roho ili uweze kutii mara moja yote ambayo Mungu anakutaka ufanye kama matokeo ya mafundisho yake ndani ya moyo wako na katika akili yako wiki hii.
Ushauri na Maombi
1
MAZOEZI
Zaburi 19:1-3
Scripture Memory
Kujiandaa kwa ajili ya darasa, tafadhali tembelea www.tumi.org/books ili kupata kazi ya kusoma ya wiki ijayo, au muulize mkufunzi wako.
Kazi ya Usomaji
Mpendwa mwanafunzi, kumbuka kwamba utaulizawa kuhusu maudhui (yaliyomo kwenye video) ya somo hili wiki ijayo. Tafadhali hakikisha unatumia muda mwingi wiki ijayo kurejelea madokezo yako, hasa yale yanayolenga dhana kuu au mawazo makuu ya somo. Pia, tafadhali soma kurasa zilizoelekezwa na kuorodheshwa hapo juu, na ufanye muhtasari wa kila ulichosoma kwa aya isiyozidi moja au mbili kwa kila ulichosoma. Usiwe na wasiwasi kuhusu kutoa muhtasari wenye taarifa nyingi; andika kile tu unachodhani ndilo wazo kuu lililojadiliwa katika sehemu hiyo ya kitabu. Tafadhali wasilisha muhtasari huu darasani juma lijalo. (Tafadhali angalia Fomu ya Ripoti ya Usomaji mwishoni mwa somo hili).
Kazi Zingine
Made with FlippingBook - Online catalogs