Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
/ 6 3
M U N G U B A B A
2. Yeye ni wa tofauti kabisa na nafsi na haiba za viumbe vyote (hujifunua kwa wanadamu; yeye si sehemu ya utendaji kazi wao au muundo wao wa ndani).
3. Mungu ni muumba ex nihilo (“kisichotokana na chochote”) wa ulimwengu.
a. Hoja hii inakanusha panentheism (kwamba Mungu anakaa katika kila kitu na kwa namna fulani ameungamanishwa na kila kitu).
b. Hii inakanusha pantheism (kwamba Mungu anahusishwa moja kwa moja na au anatokana na vitu vya ulimwengu).
2
B. Kosa la Pili: Mungu hajihusishi kwa namna yoyote na utendaji wa sasa wa ulimwengu .
1. Mungu hakuumba ulimwengu na kuuacha ujiendeshe wenyewe (kama mashine).
2. Mungu anahusika kibinafsi na kila hatua ya mambo ya wanadamu na kushikilia uumbaji kwa ajili ya kusudi lake yeye mwenyewe.
3. Hoja hii inakanusha deism (kwamba Mungu aliumba mbingu na nchi halafu akaziacha zijiwekee mipango na maelekezo yake zenyewe na kujiendesha).
C. Kosa la Tatu: kwamba hatima (Fatalism ) na bahati (chance) ndio kiini hasa cha uumbaji au historia ya mwanadamu.
1. Mungu Baba Mwenyezi ndiye anayetawala juu ya ulimwengu.
Made with FlippingBook - Online catalogs