Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook

6 8 /

M U N G U B A B A

* Tunawezaje kulielewa kwa kina fundisho la uangalizi na utunzaji wa Mungu kiasi ambacho tunaweza kutumia kweli hizi zenye nguvu kuwashauri na kuwafariji wale wanaopitia majaribu na dhiki maishani mwao?

MIFANO

Mageuzi, Uumbaji, au Nini?

Baada ya Ibada ya vijana, mmoja wa wanafunzi, Shirley, anauliza kama anaweza kuzungumza nawe kuhusu kazi ya shule anayoifanya. Kama sehemu ya insha yake ya somo la kemia, ameamua kuandika juu ya mada ya mageuzi. Hana uhakika kama anapaswa kuweka wazi katika insha hiyo kwamba yeye mwenyewe ni Mkristo, au aorodheshe tu hoja mbalimmbali zinazohusu mjadala huo. Katika kulichunguza jambo hilo, ametokea kuamini kwamba huenda sehemu fulani za dhana ya mageuzi haziko mbali sana na ukweli, lakini dhamiri yake imeshikamana na imani yake kwamba Mungu Mwenyezi pekee ndiye Muumba wa mbingu na nchi. Anaumia na kuchanganyikiwa anaposikia mwalimu wake akidai kwamba dhana ya uumbaji si sayansi bali ni mawazo ya kufikirika, lakini hataki kabisa kuharibu mahusiano yake na wengine anapowashirikisha imani yake kama mfuasi wa Yesu. Amechanganyikiwa akijaribu kufikiria ni mkakati gani hasa ungekuwa bora kwa ajili ya kazi yake. Ungemshauri vipi Shirley katika kazi yake – unadhani anapaswa kutumia mbinu gani na kushughulika vipi na kazi yake? Unapopekua rafu katika duka la vitabu lililo karibu, unakutana na kitabu kinachotengeneza hoja kwamba Holocaust (kuangamizwa kwa Wayahudi milioni sita na utawala wa Nazi kuanzia mwaka 1939-1945) ilikuwa adhabu halisi juu yao kwa kumsulubisha Masihi. Mwandishi anadai kuwa yeye ni mwanahistoria, ingawa anadokeza kuwa uchambuzi wake kwa kiasi kikubwa ni wa kitheolojia (pia anadai kuwa ni Mkristo). Tunapaswa kukielewaje kitabu hiki? Je, tunapaswa kuchukuliaje uchambuzi kama huu unao tazama matukio katika historia na kudokeza kwamba Mungu alikusudia matukio hayo yatendeke ili kutimiza kusudi la kiungu. (Kwa mfano, mwanzoni mwa karne ya 19, wengi waliamini kwamba utumwa ulikusudiwa kwa ajili ya Wamerakani wa Kiafrika, kwani, kulingana na hoja yao, walijumuishwa katika laana ya Nuhu kwa Hamu kwa kukosa kwake busara baada ya gharika [rej. Mwa. 9:24-25]). Mauaji ya Holocaust ni Adhabu

1

2

2

Made with FlippingBook - Online catalogs