Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook

7 0 /

M U N G U B A B A

Ikiwa una nia ya kufuatilia kwa kina baadhi ya mawazo ya Mungu kama Muumbaji: Uangalizi na Utunzaji wa Mungu, unaweza kujaribu vitabu hivi: Hocking, David. Who God Is. Dallas: Word Publishing, 1984. Packer, J. I. Evangelism and the Sovereignty of God. DownersGrove, IL: InterVarsity Press, 1991. Pink, A. W. The Sovereignty of God. Grand Rapids: Baker Book House, 1984. Utawala wa Mungu una aina nyingi za athari kwa kila hatua ya maisha na huduma zetu. Hii ni fursa yako tena katika somo hili kutafakari juu ya jambo au suala fulani ambalo Roho Mtakatifu anaweza kuwa anataka uchunguze kwa ajili ya huduma yako mwenyewe. Kati ya masuala yote yaliyotajwa hapo juu, ni kitu gani ambacho Roho Mtakatifu anasisitiza moyoni na akilini mwako kwa ajili ya maisha na huduma yako? Kweli gani mahususi kuhusu utunzaji, uhifadhi, na/au utawala wa Mungu zinahusiana zaidi na mzigo na mahitaji yako leo? Ni muhimu uweze kupitia tena na tena maarifa ya somo hili kwa ajili ya matumizi yako mwenyewe ya kina kwa kweli hizi. Pata wasaa wa kumtafuta Bwana na kubaini masuala au kweli ambazo zinaonekana kukaa katika ufahamu wako kuhusiana na uangalizi na utunzaji wa Mungu katika utendaji kazi wake duniani. Japokuwa tunajua wazi kwamba hatuwezi kuelewa mambo mengi mtambuka yanayohusiana na uangalizi na utunzaji wa Mungu, tunajua kwamba mioyo yetu imejaa na kutiwa moyo tunapotafakari ukuu wa Mungu katika maisha yetu. Maandiko yote yanasema wazi kwamba Mungu Baba Mwenyezi ndiye Muumba wa mbingu na nchi na kwa hiyo ulimwengu mzima ni wake, na katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake (Rum. 8:28). Bila shaka, unayo masuala na mashaka fulani yanayohitaji kusogezwa mbele ya Bwana, Mungu wa uangalizi na utawala, Mungu anayehifadhi na kuongoza. Chukua muda kuinua haja za moyo wako mbele za Bwana, kwa niaba ya maisha yako mwenyewe, wapendwa wako, na wale unaowahudumia katika huduma. Kumbuka kwamba mwalimu wako yuko tayari kuomba pamoja nawe na kukuombea katika mambo haya na mengine yanayohusiana na maisha na huduma yako.

Nyenzo na Bibliographia

Kuhusianisha Somo na Huduma

2

Ushauri na Maombi

Made with FlippingBook - Online catalogs