Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
/ 9 3
M U N G U B A B A
3. Mungu hazuiliwi na eneo fulani la kijiographia au mahali fulani.
a. Yer. 23:23-24
b. Am. 9:2-3
B. Madokezo kuhusu hali ya kiroho ya Mungu
1. Mungu hana mipaka yoyote katika uumbaji asilia wa kimwili.
2. Mungu hahitaji kukaa katika jengo, au kuishi katika mahekalu yaliyojengwa na watu, Mdo 17:24-25.
3
3. Inapotajwa “kumwona Mungu” au maumbile ya kimwili ya Mungu (k.m., mikono, miguu, macho n.k.,) ni anthropomorphisms (kuelezea kweli zinazomhusu Mungu kwa kulinganisha na sifa za kibinadamu).
4. Kuonekana kwa Mungu katika Agano la Kale kunapaswa kueleweka kama matukio ya kitheofania (kuonekana kwa Mwana wa Mungu katika wakati wa Agano la Kale, [k.m., Mwanzo18]).
II. Mungu Baba Mwenyezi ni Uzima.
A. Vipengele vya uzima wa Mungu
1. Mungu yu hai (siku zote anaishi na hataweza kuonja uharibifu).
Made with FlippingBook - Online catalogs