Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook

Jiwe Walilolikataa Waashi Limekuwa Jiwe Kuu la Pembeni

THE UR BAN

Mungu Mwana

MI N I S T R Y I NS T I TUT E h u d uma y a WOR L D IMPAC T , I NC .

u

b

c

a

h

i t

a

K

M

i

z

w

n

a

u

f

n

a

Moduli ya 10 Theolojia & Maadili

SWAHILI

K I T A B U C H A M W A N A F U N Z I

Mungu Mwana

Moduli ya 10

Theolojia na Maadili

Yesu, Masihi na Bwana wa Wote:

ALIKUJA

Yesu, Masihi na Bwana wa Wote:

ALIISHI

Yesu, Masihi na Bwana wa Wote:

ALIKUFA

Yesu, Masihi na Bwana wa Wote:

ALIFUFUKA NA ATARUDI

Mtaala huu ni matokeo ya maelfu ya masaa ya kazi iliyofanywa na taasisi ya The Urban Ministry Institute (TUMI) na haupaswi kudurufu bila idhini ya taasisi hiyo. TUMI inatoa idhini kwa yeyote anayehitaji kutumia vitabu hivi kwa ajili ya faida ya ufalme wa Mungu, kwa kutoa leseni za kudurufu za gharama nafuu. Tafadhali thibitisha kwa Mkufunzi wako ikiwa kitabu hiki kimepewa leseni ipasavyo. Kwa taarifa zaidi kuhusu TUMI na taratibu zetu za utoaji leseni, tembelea www.tumi.org na www.tumi.org/license .

Moduli ya 10 ya Mataala wa Capstone: Mungu Mwana – Kitabu cha Mwanafunzi ISBN: 978-1-62932-384-8 © 2005, 2011, 2013, 2015. Taasisi ya The Urban Ministry Institute . Haki zote zimehifadhiwa. Toleo la Kwanza 2005, Toleo la Pili 2011, Toleo la Tatu 2013, Toleo la Nne 2015. © 2023 Toleo la Kiswahili, kimetafsiriwa na Robin Mwenda na Eresh Tchakubuta. Tunatambua na kuheshimu utumishi uliotukuka wa Mtume K. E. Kisart kwa kujitolea kwake bila kukatishwa tamaa kuwafundisha viongozi katika Injili. Hairuhusiwi kunakili, kusambaza na/au kuuza vitabu hivi, au matumizi mengine yoyote pasipo idhini, isipokuwa kwa matumizi yanayo ruhusiwa kwa mujibu wa sheria ya Haki Miliki ya Mwaka 1976 au kwa idhini ya maandishi kutoka kwa mmiliki. Maombi ya idhini yatumwe katika maandishi kwa taasisi ya: The Urban Ministry Institute , 3701 E. 13th Street, Wichita, KS 67208. Taasisi ya The Urban Ministry Institute ni huduma ya World Impact, Inc Nukuu zote za Maandiko, isipokuwa kama imeonyeshwa vinginevyo, zimechukuliwa kutoka katika SWAHILI BIBLE UV050(MCR) series® Haki Miliki © 1997, iliyochapishwa na The Bible Society of Tanzania . Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote za kimataifa zimehifadhiwa.

Yaliyomo

Muhtasari wa kozi

3 5 7

Kuhusu Mkufunzi

Utangulizi wa Moduli

Mahitaji ya Kozi

15

Somo la 1 Yesu, Masihi na Bwana wa Wote: Alikuja

1

47

Somo la 2 Yesu, Masihi na Bwana wa Wote: Aliishi

2

85

Somo la 3 Yesu, Masihi na Bwana wa Wote: Alikufa

3

125

Somo la 4 Yesu, Masihi na Bwana wa Wote: Alifufuka na Atarudi

4

159

Viambatisho

/ 3

M U N G U M W A N A

Kuhusu Mkufunzi

Mchungaji Dkt. Don L. Davis ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya The Urban Ministry Institute na ni Makamu wa kwanza wa Rais wa World Impact. Alisoma katika Chuo cha Wheaton College na Chuo cha Uzamili cha Wheaton na kuhitimu kwa ufaulu wa kiwango cha juu, yaani Summa Cum Claude, katika ngazi ya Shahada (1988) na Shahada ya Uzamili (1989) katika Masomo ya Biblia na Theolojia ya Utaratibu. Alipata Shahada yake ya Uzamivu katika Masuala ya Dini (Theolojia na Maadili) katika chuo kikuu cha Iowa School of Religion. Akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi na Makamu wa Rais Mwandamizi wa World Impact , anasimamia mafunzo ya wamishonari wa mijini, wapanda makanisa, na wachungaji wa majiji, na kufanya uwezeshaji kupitia fursa za mafunzo kwa watendakazi Wakristo wa mijini katika uinjilisti, ukuaji wa kanisa, na umisheni wa upainia. Pia anaongoza Mpango wa Mafunzo Huria kwa wale wanaosoma wakiwa mbali, vilevile anawezesha Mafunzo ya Kiuongozi kwa mashirika na madhehebu kadhaa kama Prison fellowship, The Evangelical Free Church of America na The Church of God in Christ. Dkt. Davis, ambaye ametunukiwa tuzo nyingi za ualimu na za kitaalamu, amewahi kuwa profesa na Mkuu wa vitivo katika taasisi kadhaa za kitaalamu zenye hadhi ya juu, baada ya kuhadhiri na kufundisha kozi za dini, theolojia, falsafa, na mafunzo ya Biblia katika taasisi za elimu ya juu kama vile Chuo cha Wheaton, Chuo Kikuu cha St. Ambrose, Programu ya Shahada ya Uzamili ya Theolojia ya Chuo Kikuu cha Houston, Kitengo cha Dini cha Chuo Kikuu cha Iowa, na Taasisi ya Mafunzo ya Ibada ya Robert E. Webber. Ameandika idadi kubwa ya vitabu, mitaala, na nyenzo za kujifunzia ili kuwaandaa viongozi wa mijini, ikijumuisha mtaala wa mafunzo wa Capstone (hii ni programu mama ya TUMI yenye moduli 16 za hadhi ya mafunzo ya seminari, yanayotolewa kupitia mfumo wa elimu ya masafa), Mizizi Mitakatifu: Kidokezo cha Namna ya Kurejesha Mapokeo Makuu , ambayo inaangazia namna makanisa ya mijini yanavyoweza kufanywa upya kupitia kugundua upya imani halisi, sahihi ya kihistoria; na Mweusi na Mwanadamu: Kumgundua Upya M.L. King kama Nyenzo ya Theolojia na Maadili ya Weusi . Dkt. Davis pia ameshiriki katika mihadhara ya kitaalamu kama the Staley Lecture series, makongamano ya kufanywa upya kama Promise Keeper Rallies na miungano ya kithiologia kama The University of Virginia Lived Theology Project Series. Vilevile alipokea tuzo ya heshima ya mwanafunzi mashuhuri ( Alumni Fellow Award ) kutoka Chuo Kikuu cha Iowa cha Sanaa na Sayansi za Kiliberali mnamo 2009. Dkt. Davis pia ni mwanachama wa The Society of Biblical Literature, na The American Academy of Religion .

/ 5

M U N G U M W A N A

Utangulizi wa Moduli

Salamu, katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Utambulisho wa Yesu wa Nazareti na kazi yake bila shaka ni somo muhimu zaidi katika tafakari na huduma zote za Kikristo. Ni ukweli usiopingika kwamba haiwezekani kuhudumu katika Jina la Bwana Yesu Kristo ikiwa huduma hiyo imejengwa juu ya maoni na mitazamo potofu na ya aibu kuhusu yeye alikuwa nani (na ni nani), maisha yake yalimaanisha nini, na vile tunavyopaswa kumchukulia leo. Kuwa na ufahamu sahihi juu ya maisha yake, kifo chake, ufufuo wake, kupaa kwake, na kurudi kwake ndio msingi wa kila kitu kwetu. Moduli hii inaangazia maisha na matendo yake makuu. Kuwa mahiri katika maarifa ya kibiblia kuhusu Kristo ndio jukumu hasa la ufuasi na huduma yoyote makini, ya kweli na yenye ufanisi. Katika somo la kwanza, Yesu, Masihi na Bwana wa Wote: Alikuja , tunazingatia umuhimu wa Kanuni ya Imani ya Nikea katika masomo ya Kristolojia. Tutaangalia hasa jinsi Tamko la Imani la Nikea linavyosaidia kuboresha fikra zetu kama wahudumu wa mijini, kuhusiana na kujifunza kwetu maarifa ya kibiblia juu ya Yesu. Hili ni muhimu hasa katika maana ya kutusaidia kuiona kazi ya Kristo katika sura mbili: kunyenyekezwa kwake (yaani, kufanyika kwake mwanadamu na kufa kwake msalabani kwa ajili yetu) na kuinuliwa kwake (kufufuka kwake, kupaa kwake, na tumaini la kurudi kwake katika nguvu). Pia tutaangazia fundisho la kibiblia juu ya asili ya Yesu kama Neno au Logos aliyekuwepo kabla hajaja duniani. Tutazingatia uungu wake pamoja na mafundisho potofu mawili ya kihistoria kuhusu uungu wa Kristo, na tutahitimisha somo letu kwa kutoa maoni juu ya umuhimu wa uungu wa Yesu katika imani na ufuasi wetu. Kisha, somo letu la pili, Yesu, Masihi na Bwana wa Wote: Aliishi , linaangazia ubinadamu wa Kristo. Tutazingatia sababu zake mbili za kuja duniani: kutufunulia utukufu wa Baba na kutukomboa kutoka katika dhambi na nguvu za Shetani. Pia tutaangalia lugha ya Kanuni ya Imani kuhusu ubinadamu wa Yesu, kuchukuliwa kwa mimba yake kwa uweza wa Roho Mtakatifu na kuzaliwa na Bikira Maria, na kuchunguza baadhi ya makosa ya kihistoria yanayohusiana na kukana uungu wa Yesu au ubinadamu wake. Tutamalizia somo hili kwa kuchunguza mambo matatu muhimu ya maisha na huduma ya Yesu duniani. Hayo yanajumuisha utambulisho wake kama “Aliyebatizwa” anayejihusisha na watenda dhambi, Mtangaza Ufalme wa Mungu, akiithibitisha tena haki ya Mungu ya kuutawala uumbaji, na kama Mtumishi wa Yehova Atesekaye ambaye alikuja ili kuitoa nafsi yake iwe fidia kwa ajili ya wengi.

6 /

M U N G U M W A N A

Katika somo letu la tatu , Yesu, Masihi na Bwana wa Wote: Alikufa , tutachunguza maana za kitheolojia za unyonge na kifo cha Yesu, kushuka kwake katika utu wake wa kiungu kwa niaba yetu. Tutaangazia kunyenyekezwa kwa Yesu kwa njia ya Umwilisho (incarnation) , maisha na huduma yake, pamoja na kifo chake. Katika kuzingatia dhabihu yake pale Kalvari, tutachunguza baadhi ya mifano ya kihistoria inayosaidia kuelewa kazi yake juu ya msalaba. Hii inahusisha mtazamo wa kifo chake kama fidia kwa ajili yetu, kama upatanisho (utoshelevu wa kimungu) kwa ajili ya dhambi zetu, kama dhabihu mbadala badala yetu, kama ushindi dhidi ya shetani na kifo chenyewe, na kama upatanisho kati ya Mungu na wanadamu. Pia tutachunguza baadhi ya maoni mbadala ya kihistoria kuhusiana na kifo cha Yesu. Haya ni pamoja na kifo chake kama 1) kielelezo cha kiadili, 2) udhihirisho wa upendo wa Mungu, 3) udhihirisho wa haki ya Mungu, 4) ushindi dhidi ya nguvu za uovu na dhambi, na 5) kukidhi heshima ya Mungu. Hatimaye, katika somo letu la nne, Yesu, Masihi na Bwana wa Wote: Alifufuka na Atarudi , tunaanza kwa kuangalia vipengele mbalimbali na maana ya matukio mawili ambayo yanadhihirisha kuinuliwa kwa Kristo. Ufufuo unatumika kama uthibitisho wa Umasihi na uwana wa Yesu, na kupaa kwake kunampa Mwokozi wetu cheo cha hadhi na mamlaka kinachomruhusu kuvijaza vitu vyote kwa utukufu wake. Tunayachunguza haya kwa kuzingatia mafundisho ya kibiblia ya lugha ya Kanuni ya Imani, ambayo itatuwezesha kuelewa nia ya Mungu ya kumwinua Yesu wa Nazareti kuwa mrithi mkuu wa mambo yote kama matokeo ya kifo chake msalabani. Tutahitimisha somo letu kwa kuangalia kauli tatu za mwisho kuhusu Kristo katika Kanuni ya Imani ya Nikea. Tutachunguza kuja kwake katika utukufu, hukumu yake kwa mataifa, na tutazungumzia kwa ufupi utawala wake ujao katika Ufalme wa Mungu. Labda hakuna elimu ya fundisho la kibiblia inayoweza kulinganishwa na msisimko wa kupata ufahamu wa kina, kupitia Biblia na Kanuni ya Imani, juu ya utajiri, ajabu, na siri ya Mwana wa Mungu, Yesu wa Nazareti. Kunyenyekezwa kwake na kupaa kwake ni kiini cha Injili, na kitovu cha kujitoa kwetu, ibada na huduma zetu. Mungu atumie somo hili kuhusu mtu wake mtukufu kukuwezesha kumpenda zaidi na kumtumikia yeye ambaye ndiye pekee aliyepewa ukuu na Baba. Utukufu ni wake!

~ Mchungaji Dr. Don L. Davis

/ 7

M U N G U M W A N A

Mahitaji ya Kozi

• Biblia (kwa madhumuni ya kozi hii, Biblia yako inapaswa kuwa tafsiri [mf. BHN, SUV, NEN, SRUV, au NIV, NASB, RSV, KJV, NKJV, n.k. ikiwa utatumia Biblia ya Kiingereza], na sio Biblia iliyofafanuliwa [mf. The Living Lible, The Message ]). • Kilamoduli katikamtaalawaCapstone imeainishavitabuvyakiada ambavyo vinatakiwa visomwe na kujadiliwa katika muda wote wa kujifunza moduli husika. Tunakuhimiza kusoma, kutafakari, na kufanya kazi husika pamoja na wakufunzi wako, wasimamizi, na wanafunzi wenzako. Kutokana na uhaba wa vitabu unaoweza kujitokeza kwa sababu kadha wa kadha (k.m., kushindwa kuchapisha vitabu vya kutosha), tunaweka orodha yetu ya vitabu rasmi vya Capstone vinavyohitajika kwenye tovuti yetu. Tafadhali tembelea www.tumi.org/books ili kupata orodha ya vitabu vinavyohitajika kwa ajili ya moduli hii. • Daftari na kalamu kwa ajili ya kuchukua maelezo na kufanyia kazi za darasani. • Kelly, J. N. D. Early Christian Doctrines . 5th ed. San Francisco: HarperCollins, 1978. • -----. Early Christian Creeds . 3rd ed. London: Longman, 1972. • Kereszty, Roch and A. J. Stephen Maddux. Jesus Christ: Fundamentals of Christology . Staten Island, NY: Alba House, 2002. • Witherington, Ben. The Jesus Quest: The Third Search for the Jew of Nazareth . 2nd ed. Downers Grove: InterVarsity, 1997. • Wright, N. T. Who Was Jesus? Grand Rapids: Eerdmans, 1992. • Yoder, John Howard. Preface to Theology; Christology and Theological Method . Grand Rapids: Brazos Press, 2002.

Vitabu na nyenzo zingine zinazohitajika

Vitabu vya kusoma

8 /

M U N G U M W A N A

Muhtasari wa mfumo wa kutunuku matokeo na uzito wa gredi

Mahitaji ya Kozi

Mahudhurio na ushiriki darasani . . . . . . . 30% Mazoezi . . . . . . . . . . . . . . . . . 10% Mistari ya Kukumbuka . . . . . . . . . . . 15% Kazi za ufafanuzi wa Maandiko. . . . . . . . 15% Kazi za huduma. . . . . . . . . . . . . . 10% Usomaji na kazi za kufanyia nyumbani . . . . . 10% Mtihani wa mwisho. . . . . . . . . . . . . 10%

alama 90 alama 30 alama 45 alama 45 alama 30 alama 30

alama 30 Jumla: 100% alama 300

Mambo ya kuzingatia katika utoaji maksi

Kuhudhuria kila kipindi ni moja ya masharti ya msingi ya kozi hizi. Kukosa kipindi kutaathiri matokeo yako. Ikiwa una dharura isiyoepukika itakayokulazimu kukosa kipindi, tafadhali mjulishe mkufunzi wako mapema. Ukikosa kipindi ni jukumu lako kutafuta taarifa kuhusu kazi na mazoezi yaliyotolewa, na kuongea na mkufunzi wako pale inapobidi kufanya na kukabidhi kazi kwa kuchelewa. Sehemu kubwa ya mafunzo yanayohusiana na kozi hii hufanyika kupitia mijadala. Kwa hivyo, unahimizwa na kutarajiwa kushiriki kikamilifu katika kila kipindi cha kozi hii. Kila kipindi kitaanza na jaribio fupi kuhusu mawazo ya msingi yaliyofundishwa katika somo lililopita. Njia nzuri zaidi ya kujiandaa na majaribio haya ni kupitia Kitabu cha Mwanafunzi na daftari uliloandikia maelezo ya somo hilo lililopita. Kukariri Neno la Mungu ni kipaumbele cha msingi kwa maisha na huduma yako kama mwamini na kiongozi katika Kanisa la Yesu Kristo. Kozi hii ina mistari ya Biblia michache, lakini yenye umuhimu mkubwa katika jumbe zake. Katika kila kipindi utahitajika kukariri na kunukuu (kwa mdomo au kuandika) mistari ya Biblia uliyopewa na mkufunzi wako. Neno la Mungu ni zana yenye nguvu ambayo Mungu anaitumia ili kuwaandaa watumishi wake kwa kila kazi ya huduma aliyowaitia (2 Tim. 3:16-17). Ili kutimiza matakwa ya kozi hii, lazima uchague kifungu cha Biblia na kufanya uchambuzi wa kina (yaani, eksejesia au ufafanuzi wa Maandiko). Kazi yako iwe na kurasa tano ziliyochapwa kwa kuacha nafasi mbili kati ya mistari au kuandikwa vizuri kwa mkono, na izungumzie mojawapo ya vipengele vya nafsi na kazi ya Yesu wa Nazareti vilivyomo katika kozi hii. Ni shauku na matumaini yetu kwamba utashawishika kikamilifu na kuamini juu ya uwezo wa Maandiko kuleta badiliko

Mahudhurio na ushiriki darasani

Majaribio

Kukariri mistari ya Biblia

Kazi za ufafanuzi wa Maandiko

/ 9

M U N G U M W A N A

na athari chanya katika maisha yako na ya wale unaowahudumia. Unapoendelea kujifunza kozi hii, uwe huru kuongeza mistari kadhaa katika uchambuzi wako (takriban mistari 4-9) kuhusu jambo ambalo ungependa kujifunza kwa kina. Maelezo yote kuhusiana na kazi hii yametolewa katika ukurasa wa 10-11, na yatajadiliwa katika sehemu ya utangulizi ya kozi hii. Matarajio yetu ni kwamba wanafunzi wote watatumia mafunzo haya kivitendo katika maisha yao na katika majukumu yao ya kihuduma. Mwanafunzi atakuwa na jukumu la kufikiria namna ya kufanya mafunzo ya huduma kwa vitendo kwa kutumia kanuni alizojifunza katika mazingira halisi ya huduma. Maelezo ya namna ya kufanya mafunzo kwa vitendo yanapatika katika ukurasa wa 12, na yatajadiliwa katika kipindi cha utangulizi wa kozi. Mkufunzi wako anaweza kutoa kazi za darasani na kazi za nyumbani za aina mbalimbali wakati wa vipindi vya masomo au anaweza kuziandika katika Kitabu cha Mwanafunzi ulichonacho. Ikiwa una swali lolote kuhusu kile kinachohitajika kuhusiana na kazi hizi au muda wa kuzikusanya, tafadhali muulize mkufunzi wako. Ni muhimu kwa kila mwanafunzi kusoma maeneo yote ambayo inampasa kusoma katika vitabu husika vya kozi hii au katika Maandiko Matakatifu ili kujiandaa kwa ajili ya mijadala darasani. Tafadhali hakikisha unajaza na kukabidhi kwa Mkufunzi wako “Fomu ya Ripoti ya Usomaji” iliyomo katika Kitabu cha Mwanafunzi, kila wiki. Kutakuwa pia na fursa ya kupata alama za ziada endapo utasoma zaidi ya ulivyoagizwa. Mwishoni mwa kozi, Mkufunzi wako atakupa mtihani wa mwisho utakaofanyia nyumbani. Katika mtihani huu hautaruhusiwa kutumia vitabu vyako vya kozi hii isipokuwa Biblia. Utaulizwa swali ambalo litakusaidia kutafakari juu ya yale uliyojifunza katika kozi na namna yanavyoathiri mfumo wako wa fikra na utendaji wako katika huduma. Utakapokabidhiwa mtihani wa mwisho, mkufunzi wako atakupa taarifa zaidi kuhusu tarehe za kukamilisha na kukabidhi mtihani wako na kazi nyinginezo.

Kazi za huduma

Kazi za darasani na za nyumbani

Kazi za usomaji

Mtihani wa mwisho wa kufanyia nyumbani

Gredi za ufaulu

Mwishoni mwa kozi hii, gredi zifuatazo zitatolewa na kuhifadhiwa kwenye mbukumbu za kila mwanafunzi. A – Bora D – Inaridhisha B – Nzuri sana F – Hairidhishi (Feli) C – Nzuri I – Isiyokamilika

1 0 /

M U N G U M W A N A

Matokeo ya mwisho wa kozi yatatolewa katika mfumo wa gredi kwa kutumia skeli ya kutunuku matokeo kwa mtindo wa herufi zenye alama chanya na hasi, kisha alama za gedi yako ya ufaulu katika kazi mbali mbali zitajumlishwa na kugawanywa kwa idadi ya kazi na vipimo vingine husika ili kupata wastani wa matokeo yako ya mwisho. Kuchelewesha au kushindwa kabisa kukabidhi kazi zako kutaweza kuathiri matokeo yako. Hivyo, ni vyema kupangilia shughuli na muda wako mapema na kuwasiliana na mkufunzi wako endapo kutakuwa na changamoto yoyote. Kama sehemu ya ushiriki wako katika moduli hii ya Mungu Mwana ya mataala wa Capstone , utahitajika kufanya kazi ya ufafanuzi (uchunguzi wa ndani ya Maandiko yenyewe) wa mojawapo ya vifungu vifuatavyo vya Maandiko:  Yohana 1:14-18  Tito 2:11-14  Waebrania 1:5-14  Waebrania 2:14-17  Wakolosai 1:13-20  1 Timotheo 3:16  Wafilipi 2:5-11 Kusudi la kazi hii ya ufafanuzi (eksejesia) ni kukupa fursa ya kufanya uchunguzi wa kina wa kifungu muhimu kimojawapo kinachozungumza juu ya asili na kazi ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. Uongozi wa Kikristo kimsingi umejengwa juu ya kweli kuhusu Yesu. Haiwezekani wala haiaminiki kwamba mtu anaweza kuwa mhudumu mzuri wa Injili huku akiwa na ufahamu potofu, wa chini na wa aibu kuhusu Yesu. Kwa maana moja, makosa katika fundisho hili ni hatari sio tu katika eneo la imani, lakini pia yanalemaza katika eneo la ufuasi, huduma, na utumishi. Katika Wakolosai, Paulo anasisitiza kwamba Yesu Kristo pekee ndiye kiini cha huduma yoyote; “...ambaye sisi tunamhubiri habari zake tukimwonya kila mtu, na kumfundisha kila mtu katika hekima yote, tupate kumleta kila mtu mtimilifu katika Kristo” (Kol. 1:28). Kuinuka na kuanguka kwa huduma ya Kikristo kunategemeana na kuwepo au kutokuwepo kwa mwitikio sahihi, wa kibiblia, na wenye kicho cha maisha kwa Maandiko kuhusiana na uungu na ubinadamu wa Yesu, Mwana wa Mungu. Kwa hiyo, kazi hii itakupa fursa ya kutumia mojawapo ya maandiko hapo juu kama msingi wa kuchunguza ufahamu wako juu ya uhusiano wa andiko husika na Yesu Kristo. Unaposoma moja ya maandiko hapo juu (au maandiko ambayo wewe na Mkufunzi wako mtakubaliana ambayo yanaweza kuwa hayapo kwenye orodha hii), tunatumai kuwa uchambuzi wako wa maandiko hayo utakuwekea wazi zaidi asili ya utukufu wa mtu huyu ambaye tumejitolea maisha yetu yote kumtumikia na Kazi ya Ufafanuzi wa Maandiko (Eksejesia)

Dhumuni

/ 1 1

M U N G U M W A N A

kumwakilisha. Hakika, kuwa kiongozi wa kiroho ni kuwa kama Kristo mwenyewe (1 Kor. 11:1; Flp. 2:5; Rum. 8:29). Shauku yetu ni kwamba Roho Mtakatifu akupe kumfahamu Kristo ili uweze kumpenda zaidi katika roho na kweli, kumtii kwa moyo wote katika mwenendo wako binafsi wa ufuasi, na kumtumikia kwa furaha kama kiongozi mtumishi katika nafasi ambayo Mungu amekupa katika kanisa na huduma yako. Hii ni kazi ya kujifunza Biblia, na ili kufanya kazi ya eksejesia, ni lazima udhamirie kuelewa maana ya andiko husika katika muktadha wake. Ukishajua andiko lilimaanisha nini kwa wasomaji wake wa kwanza, unaweza kupata kanuni zinazotuhusu sisi sote leo, na kuzihusianisha kanuni hizo na maisha. Mchakato wa hatua tatu rahisi unaweza kukuongoza katika jitihada zako binafsi za kujifunza kifungu cha Biblia: 1. Je, Mungu alikuwa akisema nini kwa watu katika muktadha wa asili wa andiko husika ? 2. Ni kanuni gani ambazo andiko hili linafundisha ambazo ni kweli kwa watu wote kila mahali, ikiwa ni pamoja na sisi leo ? 3. Ni kitu gani Roho Mtakatifu ananiagiza kufanya kupitia kanuni hii, leo, katika maisha na huduma yangu ? Baada ya kuwa umeyajibu maswali haya katika kujifunza kwako kibinafsi, hapo sasa utakuwa tayari kuendelea kuandika ulichokigundua katika kazi uliyopewa. Angali hapa chini mfano wa muhtasari wa kazi yako: 1. Eleza kile unachoamini kuwa ndio mada kuu au wazo kuu la andiko ulilochagua. 2. Eleza kwa muhtasari maana ya andiko hilo (unaweza kufanya hivi katika aya mbili au tatu, au, ukipenda, kwa kuandika ufafanuzi mfupi wa mstari kwa mstari juu ya kifungu husika). 3. Eleza kanuni kuu moja hadi tatu au maarifa ambayo kifungu hiki kinatoa kuhusu Yesu Kristo na kazi yake. 4. Eleza jinsi kanuni moja, kadhaa, au zote zinaweza kuhusiana na yafuatayo:

Mpangilio na muundo

a. Kiroho chako binafsi na namna unavyotembea na Kristo b. Maisha na huduma yako katika kanisa lako la mahali pamoja c. Hali au changamoto katika jamii yako kwa ujumla.

1 2 /

M U N G U M W A N A

Kwa msaada au mwongozo, tafadhali uwe huru kusoma vitabu vya rejea vya kozi hii na/au vitabu vya mafafanuzi ( commentaries ), na kutumia maarifa yaliyomo katika vyanzo hivyo katika kazi yako. Unapotumia maarifa au mawazo ya mtu mwingine kujenga hoja zako, hakikisha unatambua kazi za waandishi husika kwa kutaja vyanzo vya taarifa hizo. Astahiliye heshima apewe heshima yake. Tumia marejeleo ya ndani ya maandishi ( in-text-refences ), tanbihi ( footnotes ), au maelezo ya mwisho ( endnotes ). Njia yoyote utakayochagua kutaja rejea zako itakubalika, ilimradi 1) utumie njia hiyo moja katika kazi nzima, na 2) uonyeshe pale unatumia mawazo ya mtu mwingine, na umtambue mwandishi husika kwa kumtaja. (Kwa maelezo zaidi, angalia katika Kiambatisho cha Namna ya Kuandika Kazi Yako: Mwongozo wa Kukusaidia Kutambua Waandishi wa Vitabu vya Rejea .) Kabla hujakabidhi kazi yako, hakikisha inasifa zifuatazo: • Imeandikwa au kuchapwa vizuri na inasomeka na kueleweka. • Ni uchambuzi wa mojawapo ya vifungu hapo juu. • Imekusanywa kwa wakati (haijacheleweshwa). • Ina urefu wa kurasa 5. • Inafuata muhtasari au mpangilio uliotolewa hapo juu, na imeandikwa kwa namna ambayo msomaji ataweza kuelewa. • Inaonyesha jinsi kifungu husika kinavyohusiana na maisha na huduma leo. Usiruhusumaagizo haya yakuogopeshe; hii ni kazi ya kujifunza Biblia! Unachohitaji kuonyesha katika kazi hii ni kwamba ulisoma andiko husika, umeeleza kwa muhtasari maana yake, ukaweza kupata kanuni chache muhimu kutoka katika andiko hilo, na kuzihusianisha na maisha na huduma yako mwenyewe. Kazi ya ufafanuzi inabeba alama 45 na inawakilisha 15% ya jumla ya maksi zako, hivyo hakikisha kwamba unaifanya kazi yako kuwa bora na yenye maarifa ya kutosha ya Neno la Mungu.

Utoaji maksi

Kazi ya huduma

Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo (Waebrania 4:12). Mtume Yakobo anaweka msisitizo zaidi juu ya kuwa watendaji wa Neno la Mungu, sio wasikiaji tu, tukijidanganya wenyewe. Tunahimizwa kulifanyia kazi, kulitii. Anaongeza kusema kwamba kupuuza nidhamu hii ni sawa

Dhumuni

/ 1 3

M U N G U M W A N A

na sisi kujitazama sura zetu za asili katika kioo na mara tunapoondoka tunasahau asili yetu (sis ni nani) na tulichokusudiwa kuwa. Katika kila hali, mtendaji wa Neno la Mungu atabarikiwa katika kila atendalo (Yakobo 1:22-25). Shauku yetu ya dhati ni kwamba uweze kutumia maarifa unayojifunza kwa vitendo, ukiihusianisha elimu hii na masuala na mahitaji halisi katika maisha yako binafsi, na huduma yako ndani ya kanisa lako na kupitia kanisa lako. Kwa sababu hiyo, kama takwa mojawapo muhimu la kukamilisha moduli hii, utatakiwa kufikiria namna ya kufanya mafunzo ya huduma kwa vitendo ambapo utaweza kuwashirikisha wengine sehemu ya maarifa ambayo umejifunza katika kozi hii. Kuna njia nyingi ambazo unaweza kutumia kutimiza takwa hili la kujifunza kwako. Unaweza kuchagua kuwa na muda wa kujifunza na mtu binafsi, kutumia madarasa ya Shule ya Jumapili, vikundi vya vijana au watu wazima, au hata kwa kupata nafasi ya kuhudumu mahali fulani. Unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha unajadili na hadhira baadhi ya maarifa uliyojifunza kutoka darasani. (Bila shaka, unaweza kuchagua kuwashirikisha baadhi ya maarifa kutoka katika kazi yako ya Kieksejesia ya moduli hii). Uwe huru na tayari kubadilika na kuendana na mazingira yoyote unapofanya kazi yako. Ifanye iwe yenye ubunifu na inayoruhusu kusikiliza mitazamo tofauti kwa nia ya kujifunza. Fanya uchaguzi mapema kabisa kuhusu aina ya muktadha ambao unatamani kutumia kushirikisha watu wengine maarifa haya na kisha mshirikishe Mkufunzi wako juu ya maamuzi hayo. Panga hayo yote mapema na epuka kusubiri dakika za mwisho kuamua na kutekeleza kile unachotaka katika kazi yako. Baada ya kutekeleza kazi yako, andika kwa ufupi (ukurasa mmoja) tathmini ya kazi yako na umkabidhi mkufunzi wako. Mfano wa muhtasari wa Kazi ya Huduma ni kama ifuatavyo: 1. Jina lako 2. Eneo ulilolitumia na hadhira uliyowashirikisha. 3. Muhtasari kidogo namna muda ulivyoenda, namna ulivyojisikia na namna watu walivyoitikia. 4. Ulijifunza nini kupitia mchakato mzima wa kazi yako. Kazi ya huduma inabeba alama 30 ambazo zinawakilisha 10% ya jumla ya maksi zako, hivyo hakikisha unashirikisha yale uliyojifunza kwa ujarisi na ripoti yako iwe yenye kueleweka vizuri.

Mpangilio na muundo

Utoaji maksi

/ 1 5

M U N G U M W A N A

Yesu, Masihi na Bwana wa Wote Alikuja

S O M O L A 1

Karibu katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Baada ya kusoma, kujifunza, kushiriki katika mijadala, na kutendea kazi yaliyomo katika somo hili, utakuwa na uwezo wa: • Kueleza umuhimu wa Kanuni Imani ya Nikea katika elimu ya Kristo (Kristolojia). • Kufafanua kwa umakini mada ya Kristolojia na kuongelea umuhimu wake kwa ujumla katika kuandaliwa kwetu kama viongozi katika Kanisa. • Kuonyesha kwa usahihi jinsi Kanuni ya Imani ya Nikea inavyosaidia kuboresha fikra zetu kama wahudumu wa mijini, kuhusiana na kujifunza kwetu maarifa ya kibiblia juu ya Yesu. Hili ni muhimu hasa katika maana ya kutusaidia kuiona kazi ya Kristo katika sura mbili: kunyenyekezwa kwake (yaani, kufanyika kwake mwanadamu na kufa kwake msalabani kwa ajili yetu), na kuinuliwa kwake (kufufuka kwake, kupaa kwake, na tumaini la kurudi kwake katika nguvu). • Kuelezea njia ambazo somo la Kristolojia linaweza kuwa msaada wa pekee sana leo kwa watu kama sisi tunaofanya kazi katika jamii za mijini, kuona namna ambavyo ufahamu mpya juu ya Kristo unavyoweza kutuwezesha kuudhihirisha vyema zaidi na upendo wa Mungu kwa wanadamu, na ahadi yake tukufu ya ufalme. • Kuelezea kwa usahihi vipengele muhimu vya asili ya Yesu kabla hajaja duniani, kama Neno au Logos aliyekuwepo hapo awali, kwa kutumia Kanuni ya Imani ya Nikea kama ufunguo wa kuuelewa uungu wa Yesu. • Kuonyesha njia tatu tofauti ambazo uwepo wa Yesu unaonekana katika Maandiko: kwanza kama Mungu Mwana, nafsi ya kiungu aliye sawa na Mungu, kama Yule Anayetarajiwa katika unabii wa Agano la Kale kuhusu Masihi, na kisha kama Neno la Mungu Aliyefanyika Mwili, Mungu katika umbo la mwanadamu. • Kutoa maelezo ya kukanusha uzushi mkuu wa kihistoria kuhusu uungu wa Kristo, na kutoa maoni juu ya umuhimu wa uungu wa Yesu kwa imani yetu na ufuasi.

Malengo ya Somo

1

1 6 /

M U N G U M W A N A

Bwana wangu na Mungu wangu!

Ibada

Yohana 20:19-29 - Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu. 20 Naye akiisha kusema hayo, akawaonyesha mikono yake na ubavu wake. Basi wale wanafunzi wakafurahi walipomwona Bwana. 21 Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi. 22 Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu. 23 Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa. 24 Walakini mmoja wa wale Thenashara, Tomaso, aitwaye Pacha, hakuwako pamoja nao alipokuja Yesu. 25 Basi wanafunzi wengine wakamwambia, Tumemwona Bwana. Akawaambia, Mimi nisipoziona mikononi mwake kovu za misumari, na kutia kidole changu katika mahali pa misumari, na kutia mkono wangu katika ubavu wake, mimi sisadiki hata kidogo. 26 Basi, baada ya siku nane, wanafunzi wake walikuwamo ndani tena, na Tomaso pamoja nao. Akaja Yesu, na milango imefungwa, akasimama katikati, akasema, Amani iwe kwenu. 27 Kisha akamwambia Tomaso, Lete hapa kidole chako; uitazame mikono yangu; ulete na mkono wako uutie ubavuni mwangu, wala usiwe asiyeamini, bali aaminiye. 28 Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu! 29 Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki. Kabla ya sisi kama viongozi na watumishi wa Kristo kumtumikia Bwana wetu kwa kuwatumikia wengine, kwanza kabisa na zaidi ya mambo yote, sisi ni watu wa ibada. Kumpenda Bwana Mungu wetu ndio Amri Kuu na ya kwanza (taz. Mt. 22:30 na kuendelea), na wale wanaompenda Bwana kweli bila masharti wataleta athari njema katika familia zao na kwa marafiki, washirika na wafanyakazi wenza, majirani, na hata maadui zao. Kiini cha aina hii ya athari ni nini? Katika kisa hiki, Tomaso aitwaye Pacha, mmoja wa wanafunzi wa Yesu, anafunua nguvu ya ufunuo wa kweli wa Yesu Kristo katika kuleta matokeo. Akiwa amejaa hofu na mashaka kwa sababu hakuwepo wakati Kristo alipowatokea wanafunzi wake baada ya kufufuka, Tomaso asema kwa msisitizo kwamba hataamini pasipo uthibitisho thabiti wa kisayansi wa ufufuo wa Bwana. Akiwa na uzito na kusita kwingi kukumbatia ushuhuda wa wanafunzi wenzake, aliweka wazi kigezo cha uthibitisho ambao ungeishurutisha imani yake. “ Nisipoziona mikononi mwake kovu za misumari, na kutia kidole changu katika mahali pa misumari, na kutia mkono wangu katika ubavu wake, mimi sisadiki hata kidogo .” Kigezo cha juu, kwa kweli, kwa mfuasi mchanga na mgumu! Yesu anatowakea tena wanafunzi, wakati huu Tomaso akiwepo. Yesu anatimiza waziwazi kigezo kilichowekwa na Tomaso: “ Lete hapa kidole chako; uitazame mikono yangu; ulete na mkono wako uutie ubavuni mwangu, wala usiwe asiyeamini, bali aaminiye .” Jibu la Tomaso linaonyesha namna ambavyo mashaka yake juu ya uhalisi wa ufufuo wa Yesu yaliyeyuka katika dakika moja iliyoghubikwa na kutambua, upendo, na

1

/ 1 7

M U N G U M W A N A

shauku. Kwa mtazamo wangu , jibu lake linapaza sauti kuhusu kusudi na nia ya elimu yoyote ya kweli ya Kristo katika mtazamo wa kitheolojia: “ Bwana wangu na Mungu wangu! ” Kilichoanza kwa Tomaso kama aina ya utafiti wa kiakili wenye ukaidi kuhusiana na uthibitisho wa kimwili juu ya ufufuo wa Yesu kiligeuzwa kuwa shauku iwakayo moto ya mfuasi ambaye mshangao wake unaonyesha maana halisi ya uchunguzi wa kikristolojia. “ Bwana wangu na Mungu wangu! ” Hili litakuwa ungamo la kweli, la uaminifu, na la papo hapo la kila mtu ambaye anautazama kwa umakini ukweli kuhusu Yesu wa Nazareti na, kutoka ndani ya nafsi yake, akatokea kumwona jinsi alivyo kweli kweli. Ni Roho wa Mungu pekee anayeweza kumwezesha mwanamume au mwanamke yeyote au mtoto kumwona Bwana Yesu kweli kweli; lakini, kama atafanya hivyo na kusalimisha moyo wake kwa ufunuo huo, ataungana na ukiri wa Tomaso katika maungamo binafsi ambayo yataongoza kwenye kazi, kujidhabihu, na ujasiri uleule anapotambua kwamba Mwokozi huyu mnyenyekevu lakini aliyeinuliwa, kwa kweli, ni Bwana wake na Mungu wake. Mungu na aiangazie mioyo yetu na akili zetu kupitia Maandiko, tumwone Yesu wa Nazareti jinsi alivyo hakika na tukiri pamoja na Tomaso kwa sauti kama hiyo ya shangwe na uchaji kwa mlengwa mkuu wa ibada yetu na Kiongozi wa huduma zetu: “ Bwana wangu na Mungu! ” Baada ya kutamka na/au kuimba Kanuni ya Imani ya Nikea (katika kiambatisho), sali sala ifuatayo: Mungu wa neema, Neno lako la milele alivaa mwili kati yetu pale Mariamu alipoyatoa maisha yake kulitumikia kusudi lako. Andaa mioyo yetu kwa ajili ya ujio wake tena; tufanye tuwe imara katika tumaini na waaminifu katika utumishi ili tuweze kuupokea ujio wa Ufalme wake, kwa ajili ya Kristo mtawala juu ya vyote, anayeishi na kutawala pamoja nawe na Roho Mtakatifu, Mungu mmoja, sasa na hata milele. Amina

1

Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi

~ Presbyterian Church (U.S.A.) and Cumberland Presbyterian Church. The Theology and Worship Ministry Unit. Book of Common Worship. Louisville, KY: Westminister/John Knox Press, 1993. p. 177.

Hakuna jaribio katika somo hili.

Jaribio

Hakuna Maandiko ya kukariri katika somo hili.

Mazoezi ya Kukariri Maandiko.

Hakuna kazi katika somo hili.

Kazi za kukusanya

1 8 /

M U N G U M W A N A

MIFANO YA REJEA

Unahitaji Kuwa na Uwiano Mzuri

Katikamaoni yaokuhusiana namtazamounaomuonaKristokama kiini chamambo yote kwa habari ya ibada na huduma ya Kikristo, baadhi wamedai kwamba ni lazima kuwe na “mtazamo wenye uwiano mzuri.” Mtazamo kama huo unajengwa juu ya dhana kwamba ingawa kutafuta ufahamu wa kina juu ya Yesu wa Nazareti ni muhimu kwa ufuasi katika Kristo, haisaidii kusisitiza sana hili (au fundisho lingine lolote) pasipo kuwekea mkazo mafundisho mengine. Dhana ya Christomonism ni dhana inayoamini kwamba mtu anaweza kuwekea mkazo zaidi elimu juu ya Yesu kiasi cha kukosa kabisa uwiano katika kujifunza, na kushindwa kuzingatia maarifa mengine muhimu ya Maandiko, na hata kuhusika katika makosa na tafsiri potofu ya Maandiko na mapokeo ya Kanisa. Elimu juu ya Yesu lazima iwekwe katika nafasi yake ifaayo ya uwiano katika safu nzima ya mafundisho ya Kikristo. Je, unaweza kusema ni nafasi gani inayofaa ya kumjifunza na kumjua Kristo katika mtazamo wenye “uwiano” katika ufahamu wa mafundisho ya Kikristo? Rabi mmoja, akizungumza kuhusu mjadala baina ya Wakristo na Wayahudi katika hotuba yake chuo kikuu, alitoa maelezo yake juu ya dai la kwamba Yesu wa Nazareti ndiye njia pekee ya kuwa na uhusiano na Mungu. Baada ya kueleza kwa undani namna ambavyo Ukristo kwa kiwango kikubwa unategemea historia, imani, na Maandiko ya dini ya Kiyahudi, rabi huyo, kwa ufasaha na kwa shauku, aliwashutumu wale wa jumuiya ya Wakristo wa Kiinjili kuwa watu wa mtazamo finyu, wanaojikweza, na hata wengine kuwa wapenda chuki. “Inawezekanaje hata wanajidhania kwamba wao ndio dini pekee ya kweli katika ulimwengu ambao umeteswa na kusambaratishwa kwa sababu ya ubaguzi na ukatili wa kidini. Aina hii ya madai ya haki za kipekee kwa Mungu huleta migawanyiko na migogoro kati ya watu wa Mungu. Wanathubutu vipi kusema kwamba Yesu wa Nazareti ndiye njia pekee ya kwenda kwa Mungu! Hiyo si chochote isipokua ni imani ya kihafidhina yenye roho mbaya!” Je, unaichukuliaje “kashfa ya upekee” inayotawala sasa katika nyanja ya taaluma ya kidini, yaani, “kashfa” ya ukiri wa Kikristo kwamba imani katika Yesu ndio njia pekee ya kuwa na uhusiano na Mungu ? “Huo ni msingi wa imani ya kihafidhina yenye roho mbaya!”

1

1

2

Ni wakati wa kusonga mbele !

Wengi katika makanisa yetu ya Kikristo leo wanaamini kwamba enzi ya mafundisho ya Kikristo imekwisha. Kwa hili hawamaanishi kwamba kujifunza mafundisho ya Kikristo si muhimu hata kidogo au kwamba Wakristo hawapaswi kutamani kuwa na ujuzi. Badala yake, wanasisitiza kwamba ulimwengu umechoka kusikia juu ya mabishano ya kale kuhusu yale wanayoyaona kuwa mizozo isiyo na umuhimu

3

/ 1 9

M U N G U M W A N A

kuhusiana na mambo madogo madogo ya kimafundisho. Badala ya kujikita katika mijadala isiyo na afya na ya kuchosha kuhusu migogoro ya kitheolojia ya siku za kale, tunahitaji kujihusisha na kujiwekeza katika masuala muhimu ya muktadha na wakati wetu. Hoja yao ni rahisi na ya kueleweka. Kwa kuwa watu wengi hawajali sana kuhusu migogoro ya kale ambayo walikuwa nayo watu fulani kuhusiana na asili na maisha ya Kristo, ambao historia zao hazifahamiki vizuri sana leo, pengine hatupaswi kutumia muda mwingi kwenye mimbari na mawasilisho yetu juu ya hayo. Tunahitaji kuzungumza mambo ya uhakika, ya kisasa, na yenye umuhimu katika zama hizi. Wengine, wakiwa na msimamo tofauti, wanaamini kwamba kujifunza mafundisho ya Kikristo ndio msingi wa ibada, ushirika, na huduma zetu zote. Pasipo kuifahamu kweli kuhusu Kristo alikuwa nani hasa, ni nani, na atakuwa nani, hatuwezi kueneza Injili ifaavyo wala kuhudumia ulimwengu usio na Mungu. Kwa maoni yako, ni hoja ipi yenye mantiki zaidi kati ya hoja hizi?

1

Yesu, Masihi na Bwana wa Wote: Alikuja Sehemu ya 1: Dibaji ya Elimu Juu ya Kristo

YALIYOMO

Mchungaji Dkt. Don L. Davis

Kanuni ya Imani ya Nikea inatoa muhtasari kwa uwazi na kwa ufupi unaotupa ufahamu juu ya Yesu Kristo na kazi yake. Fundisho la Kristo, au “Kristolojia,” linahusisha uchunguzi wa kina wa Maandiko ya Biblia kuhusu Yesu, hasa katika maana ya kutusaidia kuiona kazi ya Kristo katika sura mbili: kunyenyekezwa kwake (yaani, kufanyika kwake mwanadamu na kufa kwake msalabani kwa ajili yetu), na kuinuliwa kwake (kufufuka kwake, kupaa kwake, na tumaini la kurudi kwake katika nguvu). Yesu Kristo ndiye msingi wa imani ya Kikristo (1Kor. 3:11). Ukristo umejengwa juu ya upekee, kwa hakika uungu, wa Yesu wa Nazareti. Kukubali fundisho hili la msingi la Maandiko kunaufanya mfumo mzima wa Kikristo wa umwilisho, miujiza, upatanisho, na ufufuo ulete maana nzuri sana. Kuikataa kweli hii kuu kunaifanya imani iporomoke na kuingia katika mkanganyiko. Wakristo wanaweza kutofautiana juu ya namna ya ubatizo, juu ya nafasi ya wanawake katika kanisa, au juu ya maelezo ya unabii. Lakini Wakristo wa kweli, bila kujali madhehebu yao, wanakubaliana kwamba kila kitu kinategemea uungu wa Kristo.

Muhtasari wa Sehemu ya 1

~ Bruce Demarest, Jesus Christ: The God-Man . Eugene, OR: Wipf and Stock Publishers, 1978. p. 28.

2 0 /

M U N G U M W A N A

Lengo letu katika sehemu hii, Dibaji ya Elimu Juu ya Kristo , ni kukuwezesha kuona kwamba: • Kanuni ya Imani ya Nikea ina umuhimu mkubwa kwetu tunapochunguza kile ambacho Maandiko yanafundisha kuhusu Kristo, kwa lugha rasmi “Kristolojia.” • Fundisho la Kristolojia lina umuhimu mkubwa katika mafunzo yetu kama viongozi katika Kanisa, hasa kwa jinsi linavyosaidia kuweka msingi thabiti wa uelewa wetu wote wa hadithi na imani ya Kikristo. • Kanuni ya Imani ya Nikea inatengeneza fikra zetu kuhusiana na Yesu na kazi yake, hasa katika namna inavyounda mtazamo wetu kwa habari ya kazi ya Kristo kama mitazamo miwili inayohusiana : kunyenyekezwa kwake (yaani, kufanyika kwake mwanadamu na kufa msalabani kwa ajili yetu) na kuinuliwa kwake (kufufuka kwake, kupaa kwake, na tumaini la kurudi kwake katika nguvu). • Elimu mpya ya Kristolojia inaweza kuwawezesha watenda kazi na wahudumu Wakristo wa mijini kudhihirisha vyema zaidi upendo wa Mungu kwa wanadamu, na kutoa ushahidi wa kuvutia zaidi kuhusu ahadi yake tukufu ya ufalme.

1

I. Umuhimu wa Kanuni ya Imani ya Nikea katika Elimu ya Kristolojia

Muhtasari wa Sehemu ya 1 ya Video

A. Ufafanuzi wa Kristolojia

1. Christos = Masihi, Kristo, mpakwa mafuta; logos = elimu ya, maarifa ya

2. Nafsi ya Kristo ni kitovu cha imani ya Kikristo kwa namna ya kipekee tofauti na dini nyingine. Uhusiano wa karibu wa Kristo na Ukristo ni mojawapo ya sifa bainifu za dini ya Kikristo. Ukiondoa jina la Buddha kutoka kwenye Ubuddha na kumuondoa mjumbe wake katika mfumo wa imani hiyo; kama utamuondoa Muhammad kutoka kwenye Uislamu, au Zoraster kutoka kwenye dini ya kihajemi ya zamani, fundisho zima la dini hizi bado litabaki salama. Thamani ya kimatendo ya dini hizi, kama ilivyo, isingehatarishwa au kupunguzwa. Lakini muondoe Yesu Kristo kwenye Ukristo, utaacha nini? Hakuna kitakachobaki!

/ 2 1

M U N G U M W A N A

Dhana nzima na nguvu ya imani ya Kikristo iko katika Yesu Kristo. Bila yeye hakuna kitu kabisa. ~ Sinclair Patterson katika William Evans. The Doctrines of the Bible . Chicago: Moody Press, 1974. p. 53.

3. Elimu kuhusu Kristo na kazi yake ni muhimu kwa kila hatua ya imani na maisha ya Kikristo.

1

a. Uzima wa milele ni kumjua Baba na Yesu Kristo (Yohana 17:3).

b. Ufahamu juu ya Mungu na mpango wake wa ukombozi umejikita katika Yesu Kristo pekee, 1 Yoh 5:20.

Umuhimu wake halisi unaweza kueleweka tu pale ambapo uhusiano wake na watu ambao alizaliwa katikati yao utaeleweka. Kupitia matukio ambyo yalianzishwa na kazi yake hapa duniani, kusudi na agano la Mungu na Israeli vinatimizwa. Yeye ndiye aliyekuja kufanya kile ambacho watu wa Agano la Kale wala wawakilishi wao wapakwa mafuta, manabii, makuhani, na wafalme hawakuweza kufanya. Lakini walikuwa wameahidiwa kwamba Mmoja ambaye angeinuka katikati yao bado angefanya yale ambayo wao wote walikuwa wameshindwa kabisa kufanya. Kwa maana hii Yesu wa Nazareti ndiye aliyepakwa mafuta kwa Roho na nguvu (Mdo. 10:38) kuwa Masihi wa kweli au Kristo (Yohana 1:41; Rum. 9:5) kwa watu wake. Yeye ndiye nabii wa kweli ( Mk. 9:7; Lk. 13:33; Yoh. 1:21; 6:14), kuhani (Yoh. 17; Waebrania), na mfalme ( Mt. 2:2; 21:5; 27:11), kama inavyoonekana, kwa mfano, katika ubatizo wake ( Mt. 3:13 na kuendelea) na namna anavyonukuu andiko la Isaya 61 (Luka 4:16-22). Katika kupokea upako huu na kutimiza kusudi hili la kimasihi, alipokea kutoka kwa watu wa wakati wake majina ya cheo cha Kristo (Mk. 8:29) na Mwana wa Daudi (Mt. 9:27; 12:23; 15:22; cf. Luka 1:32; Rum. 1:3; Ufu. 5:5). ~ R. S. Wallace. “Christology.” Elwell’s Theological Dictionary . Electronic ed. Bible Library . Ellis Enterprises, 1998-2001.

2 2 /

M U N G U M W A N A

4. “Kashfa ya upekee:” msemo unaohusishwa na imani na ukiri wa Kikristo kwamba ujuzi wa Mungu na wokovu dhidi ya dhambi unapatikana tu katika Yesu wa Nazareti, Masihi wa Waebrania.

a. Yohana 4:22

b. Warumi 9:4-5

1

c. Mwanzo 49:10

d. Isaya 2:3

5. Unachofikiria juu ya Yesu Kristo kitaamua hatima yako ya umilele na mwisho wako (Yohana 8:21-24).

B. Umuhimu wa Kanuni ya Imani kwa Kristolojia

Mungu mwenyewe alidhihirishwa katika umbo la mwanadamu kwa kusudi la kuufanya upya uzima wa milele. ~ Ignatius, (c. 105, E) 1.58.

1. Kanuni ya Imani inatupatia uwakilishi sahihi wa Mapokeo ya Kitume : “Utume.”

2. Kanuni ya Imani inatupatia muhtasari mfupi wa mafundisho ya Biblia .

David W. Bercot, ed. A Dictionary of Early Christian Beliefs . Peabody: Hendrickson Publishers, 1998. uk. 93.

3. Kanuni ya Imani inatupatia kiwango cha kuaminika cha sifa na vigezo vya kiinjili vya viongozi wa Kanisa .

/ 2 3

M U N G U M W A N A

II. Mitazamomiwili yaUfunuowaKristo: KunyenyekezwanaKuinuliwa kwa Mungu Mwana (Flp. 2:5-11 kama Kielelezo cha Kristolojia)

A. Mtazamo wa kwanza: kunyenyekezwa kwa Kristo ( kushuka kwake duniani na kufa ), Flp. 2:6-8.

Chimbuko la dini ya Wakristo ni katika Yesu Masihi. Anaitwa Mwana wa Mungu Aliye Juu Zaidi. Inasemekana kwamba Mungu alishuka kutoka mbinguni. Alijitwalia na kujivika mwili kutoka kwa bikira wa Kiebrania. Na Mwana aliishi ndani ya binti wa binadamu. ~ Aristides. (c. 125, E) 9. 265. Ibid. uk. 93-94.

1. Mungu wa milele wa mbinguni katika nafsi ya Mungu Mwana alijinyenyekeza (kujifanya mtupu) kwa habari ya sifa zake za kiungu akaja duniani.

1

2. Hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho.

3. Alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu .

4. Tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu , alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, kwenye mti wa maumivu na mateso yaWarumi.

B. Mtazamo wa pili: kuinuliwa kwa Kristo ( kupaa kwake mbinguni na cheo cha ubwana ), Flp. 2:9-11.

Ewe Mungu mkuu! Ewe mtoto mkamilifu! Mwana ndani ya Baba na Baba ndani ya Mwana.... Mungu Neno, ambaye alifanyika mwanadamu kwa ajili yetu. ~ Klementi wa Aleksandria (c. 195, E) 2.215. Ibid. uk. 95.

1. Mwana wa Mungu aliyenyenyekezwa na kusulubiwa amefufuliwa katika wafu na kuinuliwa na Baba hadi kwenye nafasi ya utukufu wa milele, heshima, na mamlaka ya kutawala kama Bwana juu ya viumbe vyote.

2. Mungu alimwadhimisha mno , akimpa jina kuu kupita majina yote katika ulimwengu wote.

3. Kwa jina la Yesu kila goti litapigwa kwa utii na kujisalimisha.

2 4 /

M U N G U M W A N A

4. Kila ulimi utakiri kwa hiari au bila kupenda kuwa Yesu ni Bwana.

5. Kuinuliwa (viumbe vyote kuinama, kuungama, na kukiri ubwana wa Yesu) kutaleta utukufu na heshima kwa Mungu Baba aliyemwinua Mwana kwa sababu ya dhabihu na utii wake.

III. Ulazima wa Kujifunza Juu ya Kristo katika Huduma na Utume Mjini

Jina la Kristo linaenea kila mahali, linaaminika kila mahali likiabudiwa na mataifa yote yaliyoorodheshwa hapo juu, na linatawala kila mahali. ~ Tertullian (c. 197, W) 3.158. Ibid. uk. 93.

1

A. Shambulio la uongo na upotofu wa kidini: kuna hitaji kubwa la watu wanaoweza kubaini uongo wa kidini wa adui leo na kuukataa kwa ujumbe wa wazi wa wokovu kwa njia ya imani katika Yesu Kristo.

1. 1 Timotheo 4:1-3

2. Kujifunza juu ya Kristo kunaweza kutupatia silaha dhidi ya kuongezeka kwa udanganyifu wa kishetani katika nyakati tulizonazo, Yoh. 8:31-32.

B. Kuchanganyikiwa kwa giza la kiroho: lipo hitaji kubwa la watu wanaoweza kuonyesha namna ambavyo Yesu wa Nazareti amethibitisha tena mamlaka na haki ya Mungu ya kutawala ulimwenguni, na jinsi anavyoweza kuleta ukombozi na ushindi kwa wote wanaomwamini .

1. 2 Timotheo 4:1-5

2. Kujifunza elimu ya Kristo kunaweza kuangusha ngome za adui na kuiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo, 2 Kor. 10:3-5.

/ 2 5

M U N G U M W A N A

C. Hitaji la wachungaji wa mijini walioandaliwa: kuna hitaji la kizazi kipya cha wachungaji wa mijini ambao wanaweza kuwakilisha maslahi ya Kristo kwa Imani, ushawishi na nguvu .

1. Yeremia 23:1-2, 4

2. Kujifunza juu ya Kristo kunaweza kuwaandaa wachungaji wa mijini kuwajenga wanafunzi wa mijini katika kweli ya Mungu na ahadi ya Ufalme wake, Kol. 2:6-10.

1

D. Kusonga mbele kwa Injili mijini: kuna hitaji kubwa la watu wanaoweza kufundisha na kumtangaza Kristo kwa nguvu na kwa uwazi katika vitongoji vya miji ambavyo havijafikiwa .

1. Matendo 1:8

2. Kujifunza juu yaKristo kunaweza kuamsha vuguvugu jipya la uinjilisti, ufuasi, na upandaji makanisa katika jamii ambazo hazijamjua Kristo!

a. Yohana 8:28

b. 1 Petro 3:18

c. Yohana 12:32

2 6 /

M U N G U M W A N A

Hitimisho

» Kristolojia ni elimu juu ya Yesu Kristo, maisha na kazi yake.

» Kanuni ya Imani ya Nikea inajenga uelewa wetu wa fundisho la Biblia kuhusu Yesu, kushuka kwake kutoka katika nafasi yake ya utukufu kuja duniani kwa njia ya Umwilisho ( kunyenyekezwa kwake), na kupaa kwake baada ya kifo na ufufuo wake hadi kufikia cheo cha kuinuliwa cha Bwana na Mtawala wa vyote ( kuinuliwa kwake). » Yesu ni Neno la Mungu aliyefanyika mwili, Masihi aliyetabiriwa katika Agano la Kale na kufunuliwa kwa njia ya Umwilisho wake kama Neno aliyefanyika mwili. Tafadhali chukua muda wa kutosha kujibu maswali haya na mengine yaliyoibuliwa na video. Elimu ya fundisho la Kristo ni muhimu kwa kila hatua ya maisha na huduma zetu kama wanafunzi wa Kristo. Kadiri tunavyoelewa utu na kazi yake kwa uwazi na kibiblia zaidi, ndivyo tunavyoweza kumwabudu na kumtumikia ifaavyo katika Jina lake. Maswali yaliyo hapa chini yameundwa ili kukusaidia kufanya muhtasari wa mambo muhimu yaliyofundishwa katika sehemu yetu ya kwanza. Jibu kwa usahihi na ujenge mawazo na majibu yako kwa kutumia Maandiko. 1. Nini maana ya “ Christos ” na “Kristolojia?” Kwa nini elimu ya Kristolojia ni muhimu sana kwa kila nyanja ya Imani na maisha ya Kikristo? 2. “Kashfa ya upekee” ni nini? Je, sisi kama waamini katika Kristo tunapaswa kuelewaje hoja ya upekee ya Yesu kuwa Bwana naMwokozi wa ulimwengu? 3. Je, inawezekana kwamba Mungu amejifunua mwenyewe pia kupitia dini na waokozi wengine na wakati huo huo kupitia maisha na kazi ya Yesu? Ni katika maana gani tunaweza kusema kwamba Yesu wa Nazareti ndiye njia ya mwisho na ya pekee ya kuwa na uhusiano na Mungu? Je, hii ina tafsiri gani kuhusiana na kazi ya kueneza Injili katika jamii zenye tamaduni nyingi mchanganyiko kama ya kwetu? 4. Kanuni ya Imani ya Nikea ina nafasi gani katika kutusaidia kuelewa asili ya utu na kazi ya Kristo? Je! Kanuni ya Imani inatusaidiaje kuelewa maandiko ya Biblia, yaani, yale madai ya Biblia ambayo ndio msingi wa Kanuni hiyo ya Imani? 5. Kwa nini ni muhimu kuruhusu Maandiko kuwa chanzo chenye mamlaka zaidi cha maarifa yote kuhusu Yesu Kristo? Je! tunapaswa kufanya nini

1

Sehemu ya 1

Maswali kwa wanafunzi na majibu

/ 2 7

M U N G U M W A N A

ikiwa tutakutana na tofauti kati ya kile ambacho Maandiko yanafundisha kuhusu Bwana Yesu na vyanzo vingine vinavyodai kuwa na mamlaka juu ya elimu ya Yesu? 6. Elezea mitazamo miwili ya kazi za Kristo zilizojumuishwa katika dhana ya “kunyenyekezwa” na “kuinuliwa.” Jibu kwa ufasaha na utumie Maandiko. 7. Toa sababu kadhaa zinazoonyesha kwa nini elimu juu ya nafsi na kazi ya Kristo ni muhimu hasa kwa wahudumu wa mijini na makanisa ya mijini.

1

Yesu, Masihi na Bwana wa Wote: Alikuja Sehemu ya 2: Kristo Kama [ Logos ] Neno Aliyekuwepo Tokea Awali

Mchungaji Dkt. Don L. Davis

Yesu wa Nazareti ni Mwana wa Mungu, na kabla ya kuja duniani kwa kusudi la kuufunua utukufu wa Mungu na kuukomboa uumbaji, alikuwepo kama Neno au Logos aliyekuwepo tokea awali. Maandiko yanafundisha kwa uwazi kuhusiana na kuwepo kwake kabla, ikijumuisha nafasi yake kama Mungu Mwana, nafsi ya kiungu aliye sawa na Mungu, Aliyetarajiwa katika unabii wa Kimasihi wa Agano la Kale, na kisha kama Mwenye mwili, Neno la Mungu aliyefanyika mwili, Mungu katika umbo la mwanadamu. Malengo yetu katika sehemu hii, Kristo Kama [Logos] Neno Aliyekuwepo Tokea Awali , ni kukuwezesha kuona kwamba: • Maandiko Matakatifu yanafundisha kwa uwazi kwamba Yesu wa Nazareti, kabla ya kuja duniani, alikuwepo akiwa mshiriki wa Uungu, Neno aliyekuwepo hapo awali au Logos. Mafundisho haya ya kibiblia yanathibitishwa kwa moyo wote katika Kanuni ya Imani ya Nikea, imani kuu ya awali ya kiekumene (ya Kanisa la ulimwengu) inayokiri kuwepo kwa Yesu Kristo kabla ya kuja duniani, na uungu wake. • Kuwepo kwa Yesu kabla kumewekwa katika njia tatu zinazohusiana na muhimu katika Maandiko: kwanza kama Mungu Mwana, mtu wa kiungu sawa na Mungu, kama Aliyetarajiwa katika unabii wa Agano la Kale kuhusu Masihi, na pia Neno la Mungu aliyefanyika mwili, Mungu katika umbo la mwanadamu. • Wakati ambapoaidha asili yaYesuya kiunguauya kibinadamu inapokataliwa au kueleweka kwa na namna potofu na za uongo, mafundisho yanayotokea

Muhtasari wa Sehemu ya 2

Made with FlippingBook - Online magazine maker