Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook
Mungu Mwana Utambulisho wa Yesu wa Nazareti na kazi yake bila shaka ni somo muhimu zaidi katika tafakari na huduma zote za Kikristo. Ni ukweli usiopingika kwamba haiwezekani kuhudumu katika Jina la Bwana Yesu Kristo ikiwa huduma hiyo imejengwa juu ya maoni na mitazamo potofu na ya aibu kuhusu yeye alikuwa nani (na ni nani), maisha yake yalimaanisha nini, na vile tunavyopaswa kumchukulia leo. Kuwa na ufahamu sahihi juu ya maisha yake, kifo chake, ufufuo wake, kupaa kwake, na kurudi kwake ndio msingi wa kila kitu kwetu. Moduli hii inaangazia maisha na matendo yake makuu, na kuwa na umahiri katika maarifa ya kibiblia kuhusu yeye ndio jukumu hasa la ufuasi na huduma yoyote makini, ya kweli na yenye ufanisi. Katika kozi hii muhimu, kwanza tunazingatia umuhimu wa Tamko la Imani la Nikea kwa masomo ya Kikristo, hasa jinsi linavyoweka kazi ya Kristo katika mitazamo miwili: kunyenyekezwa kwake (yaani, kufanyika kwake mwanadamu na kufa msalabani kwa ajili yetu) na kuinuliwa kwake (kufufuka kwake, kupaa kwake, na tumaini la kurudi kwake katika nguvu). Tutaangalia ubinadamu wa Kristo na mwelekeo wake wa pande mbili: kutufunulia utukufu wa Baba na kutukomboa kutoka katika dhambi na nguvu za Shetani. Tutachunguza uzushi muhimu unaotilia shaka asili yake ya kibinadamu, na kuchunguza matokeo ya kitheolojia ya kunyenyekezwa kwa Yesu na kifo chake, na nadharia mbalimbali za upatanisho ambazo zimetafuta kueleza maana ya kifo chake kwa ajili ya wanadamu. Hatimaye, tutazingatia vipengele vya matukio mawili ambayo yanaashiria kuinuliwa kwa Kristo, yaani, ufufuo wake na kupaa kwake kwa Baba. Tutamalizia somo letu kwa kutazama kuja kwake katika utukufu, hukumu yake kwa mataifa, na utawala wake ujao akiwa Mfalme katika Ufalme wa Mungu.
Mchungaji Dkt. Don L. Davis, (Ph.D., Chuo Kikuu cha Iowa) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya The Urban Ministry , ambayo ni huduma ya World Impact . Pia anahudumu kama Makamu wa Rais Mwandamizi wa World Impact . TUMI imejitolea kuwezesha vuguvugu za upandaji makanisa kote ulimwenguni ambazo zinawaandaa viongozi ili kuendeleza Ufalme miongoni mwa watu maskini wa mijini. World Impact ni shirika la kimisheni la Kikristo ambalo limejidhatiti kuwezesha harakati za upandaji makanisa kwa njia ya kufanya uinjilisti, kuandaa na kuwawezesha maskini katika miji ya Amerika. Maono yetu ni kusajili, kuwezesha, na kuwatuma viongozi wa mijini ambao watapanda makanisa na kuzindua harakati za upandaji makanisa ya kienyeji.
kuandaa viongozi. kuwezesha harakati.
THE URBAN MINISTRY INSTITUTE • HUDUMA YA WORLD IMPACT, INC.
Made with FlippingBook - Online magazine maker