Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook
/ 1 0 7
M U N G U M W A N A
b. Anatoa uwezekano wa msamaha (ikiwa atachagua kufanya hivyo) na anaweka muundo thabiti wa Yeye kutawala.
5. Kifo cha Yesu kinatuonyesha yale ambayo haki ya Mungu iliyojaa uadilifu itatutendea ikiwa tutaendelea kutenda dhambi.
a. Mateso ya Kristo yanaweza kutushawishi kwamba dhambi hailipi.
b. Tunaweza kusamehewa tukitubu, na utawala wa Mungu juu ya ulimwengu wake utabaki imara na thabiti.
B. Hoja dhidi ya mtazamo wa Kiserikali :
3
1. Hakuna ushahidi wa kibiblia au wa kimaandiko unaounga mkono mtazamo huu (ni tafsiri potofu tu kuhusu Isaya 42:21).
2. Ni hoja ya kimantiki tu: madai yaliyotolewa na hoja nyingine zinazotolewa kutokana na madai hayo kimsingi ni madai na hoja za kiakili na fikra za wanadamu.
3. Inakuza vibaya maana ya upendo wa Mungu pasipo kuzingatia ukweli kuhusu utakatifu wake.
C. Tunaweza kupata kweli gani kutokana na mtazamo huu?
1. Kifo cha Yesu kiliathiri utawala wa ulimwengu mzima kwa faida ya kusudi na mapenzi yake mwenyewe (Rom. 14:7-9).
2. Nguvu ya utawala wa Shetani imevunjwa kupitia kifo cha Yesu Kristo (Ebr. 2:14).
Made with FlippingBook - Online magazine maker