Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook
/ 1 0 9
M U N G U M W A N A
b. Mungu hahitaji (wala hawezi kukubali fidia kama hiyo).
c. Ibilisi alihitaji roho ya Yesu kama malipo kwa ajili ya wafungwa wa ulimwengu.
5. Ibilisi alikosea; baada ya kuachilia roho za wanadamu kupitia malipo ya nafsi ya Yesu, alipigwa na butwaa kwa sababu Yesu alifufuka katika wafu!
6. Shetani hakuufahamu vyema uwezo mkuu wa Yesu; kwa kifo na ufufuo wake, Ibilisi alipoteza uzao wote wa mwanadamu, na bado hakuweza kumshikilia Yesu kama fidia.
B. Hoja dhidi ya maoni ya Fidia :
3
1. Biblia haifundishi kwamba fidia ilihitaji kulipwa kwa Ibilisi ili kuwakomboa wanadamu.
2. Kristo alikufa badala yetu ili atukomboe kutokana na adhabu ya dhambi zetu (yaani, laana ya sheria), Gal. 3:13.
3. Upatanisho wa Kristo na mateso yake kwa ajili ya deni letu la dhambi na adhabu vilivunja nguvu ya dhambi kutushikilia kwa kila njia (sio kama deni fulani lililohitaji malipo kwa Shetani), Ebr. 2:14.
4. Kitendo cha Yeye kufanyika dhabihu badala yetu kilileta ukombozi kutoka katika utumwa wa laana, sio malipo kwa shetani.
Made with FlippingBook - Online magazine maker