Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook
1 1 6 /
M U N G U M W A N A
vile Bwana wetu alivyoteseka kwa ajili yetu. Zingatia kwa uangalifu maana hizi unapopitia dhana kuu za somo hili zilizopo hapa chini. ³ Kunyenyekezwa kwa Yesu Kristo, tukitumia maneno ya mwanatheolojia Oden, kunahusu kushuka kwake kutoka mbinguni katika utukufu wake wa kiungu, kuja duniani na kufa kwa ajili ya ulimwengu. ³ Unyenyekevu huu uliakisiwa katika kila nyanja ya Umwilisho wa Yesu na maisha ya duniani, tangu kuzaliwa kwake hadi maisha na huduma yake. Kilele cha kujishusha na unyenyekevu huu kinadhihirishwa katika mateso na kifo chake pale Kalvari. ³ Kifo cha Yesu kinaweza kutafsiriwa kupitia vipengele mbalimbali vinavyotuwezesha kuelewa mbaraka ambao mateso yake yaliutoa kwa ulimwengu. Vipengele hivi ni pamoja na dhana ya kifo cha Yesu kama fidia kwa ajili yetu, kama upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu, kama dhabihu mbadala badala yetu, kama ushindi dhidi ya ibilisi na kifo chenyewe, na kama upatanisho kati ya Mungu na wanadamu. ³ Katika historia ya Kanisa, kumekuweko na nadharia mbalimbali za upatanisho wa Yesu ambazo zimeanzishwa na kubishaniwa. Nadharia hizi mbalimbali hujikita kwenye vipengele fulani mahususi vya wokovu, na zikichukuliwa kwa pamoja zinatuwezesha kupata ufahamu mpana zaidi na uelewa wa kina wa umuhimu wa kifo cha Yesu kwa ajili yetu. ³ Baadhi ya nadharia kuu kuhusu maana ya kifo cha Yesu ni pamoja na kuona kifo chake kama 1) kielelezo cha kiadili, 2) udhihirisho wa upendo wa Mungu, 3) udhihirisho wa haki ya Mungu, 4) ushindi dhidi ya nguvu za uovu na dhambi, na 5) kukidhi heshima ya Mungu. ³ Ingawa hakuna nadharia moja kati ya hizo inayoelezea kikamilifu kifo cha Yesu, kila moja ina kweli zinazoweza kukuza uelewa wetu wa maana na ukweli wake kwa upana mkubwa zaidi. Sasa ni wakati wa kujadiliana pamoja na wanafunzi wenzako maswali uliyo nayo kuhusu kunyenyekezwa kwa Yesu na kilele cha unyenyekevu na kujishusha huko kupitia kifo chake msalabani. Kama ilivyotajwa hapo juu, bila shaka ni moja ya mada muhimu zaidi ambayo sisi kama viongozi wa kiroho tunahitaji kuweka juhudu kuielewa. Kuelewa maana ya kifo cha Yesu ndio moyo wa maungamo yetu na msukumo wa huduma yetu ya Kikristo. Bila shaka, maswali fulani yamekuja akilini mlipojadili na kusoma mawazo haya. Ni masuala gani hasa ambayo yamefunuliwa katika kujifunza kwako kuhusu kifo cha Kristo hadi sasa? Maswali
3
Kutendea kazi somo na matokeo yake kwa mwanafunzi
Made with FlippingBook - Online magazine maker