Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook

1 1 8 /

M U N G U M W A N A

Imani Isiyo na Damu?

MIFANO

Mahubiri mengi ya kisasa ya Injili yanaelekea kuwekea mkazi zaidi juu ya maadili ya imani ya Kikristo , yaani, juu ya tabia ya mahusiano na maadili yanaohusishwa na imani ya Kikristo na si juu ya mateso ya Kristo, unyenyekevu wake, maumivu yake, na kifo chake Kalvari. Makanisa mengi makubwa yanayohusishwa na mbinu za ukuaji wa Kanisa na mbinu za kisasa zaidi za ibada na ushuhudiaji yako wazi katika msisitizo wao wa kwamba kushughulika kila mara na mada za ukatili na mateso, mada za kifo na dhabihu, hakuleti ufanisi katika kuwavuna wengine. Makanisa yanayokua yanashughulika na masuala “halisi”, yanashughulikia mahangaiko na matatizo halisi ya watu, na kuzingatia ubora wa masuala ya maisha ambayo watu wengi wa Magharibi wanahangaikia siku hadi siku. Wanabainisha kwamba mchakato wa kuingia kwenye maisha yao hauwezi kuanza na mafundisho magumu juu ya damu ya Kristo iliyomwagika, badala yake, tunapaswa kuanza na masuala ya msingi zaidi kama kazi, familia, na maendeleo binafsi. Ni wakati gani tunapaswa kuwafundisha “watafutaji” wa kweli wa Mungu mafundisho yanayohusiana na msalaba wa Kristo ? Je, mafundisho hayo ni ya kutumia kujengea “msingi” au ya “kupaulia” kazi ya ushuhudiaji? Elezea jibu lako. Katika ulimwengu ambao umegawanyika kwa mizozo ya kisiasa, wahubiri wengi wa kiinjili wameazimia kutotumia mifano ya kijeshi ya Agano Jipya katika kueneza imani. Ingawa sehemu kubwa ya lugha ya Yesu na mitume imetumia mifano ya kijeshi ili kuleta maana ya maisha na utume wa Yesu, ikiwa ni pamoja na kifo chake msalabani, ni waalimu wachache sana ambao wanajitahidi kufuata mfano wao leo. Baadhi wameenda mbali na kudai kwamba kutumia lugha za picha kama hizi kuelezea asili ya imani ya Kikristo litakuwa kosa kubwa wakati kama huu, ambapo ubaguzi wa kidini, jihadi , vurugu na kutovumiliana vinafanyika kwa jina la miungu na dini. Taswira ya vita ni ukweli wa kutisha, na ambao hatupaswi kutumia bila tahadhari ya kweli. Wengine wanasema kwamba mifano hii imevuviwa na Mungu na imetolewa ili kutuwezesha kuelewa maana ya msingi ya ukombozi katika Kristo . Kwa maneno mengine, mifano ya vita ilichaguliwa kwa sababu inawasilisha asili ya kweli ya kiroho vizuri zaidi kuliko njia nyingine yoyote; Yesu alikuja ili kuziharibu kazi za shetani (1 Yohana 3:8). Ulimwengu uko vitani, na hakuna kiasi cha kukerwa kitakachobadilisha ukweli huu. Je, kutumia taswira ya vita kama nadharia ya upatanisho ni sahihi kwetu leo? Nadharia zisizosahihi kisiasa

1

3

2

Made with FlippingBook - Online magazine maker