Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook

1 2 6 /

M U N G U M W A N A

sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini 12 Usiku umeendelea sana, mchana umekaribia, basi na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru. 13 Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu. 14 Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake. Ni vigumu kukadiria jinsi ushuhuda wa mitume ulivyokuwa na nguvu katika ulimwengu wa Kirumi muda mfupi baada ya siku za ufufuo na kupaa kwa Bwana wetu. Ujumbe wa kufa, kufufuka, kupaa, na kurudi kwa Yesu ulikuwa zaidi ya matamanio ya dhehebu dogo la Kiyahudi la wafuasi waliodanganyika wa rabi aliyeshindwa. Badala yake, ujumbe wa Mnazareti uligeuka moto mkali uliowasha kila kijiji na mji ambako wafuasi wa Yeshua (Yesu) walikusanyika na kunena. Roho Mtakatifu alibadilisha kundi dogo la wanafunzi waliochanganyikiwa na wenye woga na kuwa wajumbe wa utaratibu mpya wenye kubadilisha ulimwengu ambao, wakati wowote, ulitarajiwa kufunuliwa katika wakati na mbinu ya Mungu mwenyewe. Ni maono gani yaliyowasha ushirika huo mpya, ambayo yaliwafanya kuwa moto na kuwa tayari kutoa aina za dhabihu ambazo zilikisukuma kizazi kizima kutoa ushahidi juu ya Masihi na tumaini la uzima wa milele katika jina lake? Hata usomaji wa harakaharaka wa kitabu cha Matendo ya Mitume na Nyaraka unaonyesha kwamba mtazamo wa ulimwengu wa mitume ulikuwa ni mtazamo wa wajumbe wa enzi maalum na Bwana wa enzi husika ambayo, wakati wowote, ilikuwa karibu kufunuliwa katikati ya enzi potofu na mfu. Waliishi kama watu walioamini kwa hakika kwamba Mnazareti huyu kwa hakika alikuwa Mwana wa Mungu ambaye alikuja kukomesha dhambi, kuharibu kazi ya shetani, na sasa alikuwa hai na akimimina baraka, karama na vipawa vyake ndani yao ili waweze kumwakilisha. Kwao, alikuwa Bwana kweli. Wakati wowote, angeweza kuamua kurudi (kwa idhini na amri ya Baba), na kukamilisha kazi ambayo aliianza hapa. Katika lugha kavu ya shule za theolojia, walikuwa jamii ya kieskatolojia . Hilo linamaanisha, utambulisho wao wote, mfumo wao wa kimaadili, na mtazamo wao wa ulimwengu uliundwa na ile imani yao kwamba ulimwengu mpya ulikuwa karibu kupambazuka, na kwamba wakati ulikuwa karibu (karibu sana) wa kufuniliwa kwa ulimwengu huo mpya. Siku yoyote inaweza kuwa siku yenyewe . “Na zaidi ya hayo mwaujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imefika. Kwa maana wokovu u karibu nasi sasa kuliko tulipoanza kuamini.” Imani yao ilikuwa kwamba Yesu alikuwa Masihi, kwamba alikufa na kufufuka ili kuanzisha kazi ya Mungu ya uumbaji mpya, kwamba alipaa mbinguni na hivi karibuni angerudi ili kusimamisha utawala wa Mungu duniani na kutawala akiwa Mfalme. Maono hayo yaliwasha mawazo na mioyo yao, yakawategemeza katika majaribu, na kuwachochea waende kwenye miisho ya dunia iliyojulikana wakati huo wakiwa

4

Made with FlippingBook - Online magazine maker