Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook
1 3 2 /
M U N G U M W A N A
B. Lugha ya Kanuni ya Imani na ushahidi wake katika Biblia
1. “Siku ya Tatu Alifufuka…”: ushahidi wa kihistoria wa simulizi za ufufuo (Mt. 28:1-15; Marko 16:1-11; Lk 24:1-12; Yoh. 20:1-18)
a. Ushahidi wa kihistoria kwamba Yesu alikufa kweli ni mwingi na wa wazi. (1) Kusulubiwa na kuchomwa mkuki (Yoh. 19:33-37) (2) Ombi la Yusufu wa Arimethea na kukubaliwa kuuchukua mwili wa Yesu (Mt. 27:57-58) (3) Uthibitisho wa Pilato kupitia kwa akida kwamba Yesu wa Nazareti amekufa (Mk 15:44-45) (4) Ushuhuda wa askari juu ya kifo cha Yesu (Yoh 19:33) (5) Ushuhuda wa Yesu aliyetukuzwa (Ufu. 1:17-18).
2. “Kama yasemavyo Maandiko”: utabiri wa Biblia
4
a. Nukuu ya Paulo ya Zaburi 2 na Zaburi 16 kama Maandiko yanayozungumzia ufufuo wa Yesu Kristo (Mdo 13:30-37).
b. Utetezi wa Paulo kuhusu utume wake (Mdo 26:22-23).
c. Uhakika wa ufufuo wa Mtumishi wa Yehova Atesekaye (Isa. 53:10-12).
d. Dokezo la ufufuo wa Yesu? Hos. 6:2.
Made with FlippingBook - Online magazine maker