Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook
/ 1 3 5
M U N G U M W A N A
a. Kaburi tupu: je, kuna maelezo rahisi ya kuaminika zaidi ya ufufuo zaidi ya ukweli kwamba kaburi bado ni tupu ?
b. Kutokuwepo kwa mwili wa Yesu: kwa nini wapinzani hawakuutoa mwili wa Yesu na kukiponda kikundi hiki cha wafuasi wake kwa pigo moja na kuwamaliza kabisa ?
c. Wingi wa mashahidi waliomwona Yesu Mfufuka (taz. 1 Kor. 15:3-9): ingewezekanaje watu wengi kiasi hiki wakapatana kwa ufanisi mkubwa kiasi hiki kutunga habari za uongo kuhusu kufufuka kwa Yesu ?
d. Kugeuzwa kwa wanafunzi: nini kingewafanya Mitume wahatarishe maisha yao kwa ajili ya imani ambayo walifahamu kuwa ni ya uongo ?
e. Kuundwa kwa jamii na imani ya Kikristo: hakuna sababu ya kuwepo kwake inayoonekana kuwa na maana ikiwa Kristo hakufufua .
4
f. Kuundwa kwa Agano Jipya: ikiwa Yesu angebaki kaburini, je, hadithi hii, isiyo ya kweli na ya kutunga tu, haikupaswa kufifia na kupotea kabisa muda mrefu kabla ya sasa ?
2. Ufufuo ni ishara ya nje ya uhalalisho na uthibitisho wa ushindi wa Yesu juu ya kifo, shetani, na madhara yote ya laana (1 Kor. 15:24-28).
3. Sisi wenyewe tutashiriki utukufu ule ule wa mwili ambao Yesu anao kwa sasa: miili yetu itafananishwa na mfano wake haswa.
a. Warumi 8:29
b. 1 Wakorintho 15:48-49
Made with FlippingBook - Online magazine maker