Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook

/ 1 5 3

M U N G U M W A N A

³ Ufufuo unatumika kama uthibitisho wa Umasihi na uwana wa Yesu, na kupaa kwake kunampa Mwokozi wetu cheo cha hadhi na mamlaka kinachomruhusu kujaza vitu vyote kwa utukufu wake. ³ Tukio la Kristo (yaani, kuwepo kwa Yesu kabla, maisha yake, huduma, kifo, ufufuo, na utukufu wake) linaweza kufikiriwa kwa maana ya mitazamo au mielekeo miwili, mwelekeo wa kushuka (katika unyonge au kunyenyekezwa), na kupanda (kuinuliwa). Ufufuo na kupaa vinahusishwa moja kwa moja na kuinuliwa kwa Kristo na utukufu wake. ³ Kauli tatu mahususi katika Kanuni ya Imani ya Nikea zinazungumza juu ya kazi ya Yesu duniani katika wakati ujao. ³ Kanuni ya Imani inazungumza kwamba Yesu Kristo atarudi tena katika utukufu, tendo ambalo litakuwa la ajabu kwa maana ya ukuu wa tendo lenyewe na lina umuhimu kwa wakati wa sasa katika maisha na huduma zetu. ³ Kanuni ya Imani pia inathibitisha kwamba atakuja kuhukumu mataifa, kwa maana Baba amemkabidhi Mwana hukumu yote. ³ Hatimaye, Kanuni ya Imani inakiri kwamba atatawala na Ufalme wake hautakuwa na mwisho, atatimiza unabii wa Agano la Kale na kuanzisha utawala wa Mungu katika mbingu mpya na nchi mpya. ³ Kweli hizi tatu (yaani, kuja kwake katika utukufu, hukumu yake kwa mataifa, na Ufalme wake wa milele) zinabeba maana kubwa katika maisha na huduma zetu leo. Sasa ni wakati wa kujadili pamoja na wanafunzi wenzako maswali yako kuhusu ufufuo, kupaa, na kurudi kwaBwana.Mafundishohaya yanatupa, sisi kama viongozi wa Kikristo, ujasiri na uhakikisho tunaohitaji ili kuwashirikisha Habari Njema wale wasiomjua Kristo, na vile vile kuwakuza wanafunzi ambao tunawafundisha na kuwandaa katika Kanisa. Ni maswali gani yamekuja akilini wakati tunaangazia kwa kina ushuhuda huu wa kusisimua wa Biblia kuhusu kuinuliwa na kurudi kwa Bwana wetu? Tumia maswali yaliyo hapa chini kuibua maswali yako mwenyewe kuhusu maana za kuinuliwa kwa Kristo katika maisha na huduma yako. * Kwa nini fundisho la ufufuo ni muhimu sana kwa fundisho la ufufuo wa Kristo ?

4

Kutendea kazi somo na matokeo yake kwa mwanafunzi

Made with FlippingBook - Online magazine maker