Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook

1 5 6 /

M U N G U M W A N A

ukuu wa tendo lenyewe na lina umuhimu kwa wakati wa sasa katika maisha na huduma zetu. Kisha, Kanuni ya Imani inathibitisha kwamba atakuja kuhukumu mataifa, kwa maana Baba amemkabidhi Mwana hukumu yote. Hatimaye, Kanuni ya Imani inakiri kwamba atatawala na Ufalme wake hautakuwa na mwisho, atatimiza unabii wa Agano la Kale na kusimika utawala wa Mungu katika mbingu mpya na nchi mpya. Kweli hizi tatu (yaani, kuja kwake katika utukufu, hukumu yake kwa mataifa, na Ufalme wake wa milele) zinabeba maana kubwa katika maisha na huduma zetu leo. Ikiwa utapenda kupata ufahamu wa kina zaidi kuhusu baadhi ya maarifa yaliyomo katika somo hili la Yesu, Masihi na Bwana wa Wote: Alifufuka na Atarudi , unaweza kujaribu vitabu vifuatavyo: Craig, William Lane. The Son Risen: The Historical Evidence for the Resurrection of Jesus. Chicago: Moody Press, 1981. Ladd, George Eldon. I Believe in the Resurrection of Jesus. Grand Rapids: Eerdmans, 1975. ------. The Last Things. Grand Rapids: Eerdmans, 1978. Wenham, John. Easter Enigma: Are the Resurrection Accounts in Conflict? Grand Rapids: Baker Book House, 1992. Sasa umefikia hatua katika masomo yako ambapo utatakiwa kutumia maarifa uliyoyapata katika kujifunza moduli hii kwenye mazoezi ya huduma kwa vitendo ambayo wewe na mkufunzi wako mtakubaliana. Una wajibu wa kuyafanya matokeo ya kuinuliwa kwa Kristo, ushuhuda kuhusu kufufuka na kupaa kwake, na uhakika wa tumaini la kurudi kwake viwe halisi katika maisha na huduma yako. Anza kufikiria njia zote zisizo na idadi ambazo mafundisho haya yanaweza kuathiri maisha yako ya ibada, maombi yako, mwenendo wako katika kanisa lako, mtazamo wako kazini, na kadhalika. Kilicho muhimu sasa katika masomo yako ni kutumia sehemu ya ujuzi huu katika suala halisi na eneo halisi katika maisha, kazi, na huduma yako. Kazi ya Huduma kwa Vitendo imekusudiwa kukusaidia kutendea kazi Neno ambalo umejifunza, na katika siku chache zinazofuata utakuwa na fursa ya kutumia maarifa haya na kuwashirikisha wengine katika mazingira halisi ya huduma. Mwombe Mungu akupe ufahamu wa njia zake unaposhirikisha wengine ujuzi wako kupitia kazi zako za moduli hii.

Nyenzo na Bibliografia

4

Kuhusishianisha somo na huduma

Made with FlippingBook - Online magazine maker