Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook

/ 1 6 1

M U N G U M W A N A

K I A M B A T I S H O C H A 1 Kanuni ya Imani ya Nikea

Mistari ya Kukumbuka 

Tuna amini katika Mungu mmoja, (Kum. 6.4-5; Marko 12.29; 1 Kor. 8.6) Baba Mwenyezi, (Mwa. 17.1; Dan. 4.35; Mt. 6.9; Efe. 4.6; Ufu. 1.8) Muumba wa mbingu na nchi (Mwa 1.1; Isa. 40.28; Ufu. 10.6) Na vitu vyote vinavyoonekana na visivyo onekana (Zab. 148; Rum. 11.36; Ufu. 4.11) Tuna amini katika Bwana mmoja Yesu Kristo, Mwana pekee atokaye kwa Mungu, Aliyezaliwa na Baba kabla ya nyakati zote, Mungu atokaye kwa Mungu, nuru itokayo katika nuru, Mungu wa kweli atokaye kwa Mungu wa kweli. Aliyezaliwa na si kuumbwa, Mwenye asili moja na Baba, (Yoh. 1.1-2; 3.18; 8.58; 14.9-10; 20.28; Kol. 1.15, 17; Ebr. 1.3-6) Katika yeye vitu vyote vilifanyika (Yohana 1.3; Kol. 1.16) Ambaye kwa ajili yetu na kwa ajili ya wokovu wetu alishuka kutoka mbinguni na alifanyika mwili kwa Roho Mtakatifu na bikira Mariamu na kuwa Mwanadamu. (Mt. 1.20-23; Yohana 1.14; 6.38; Luka 19.10) Ambaye kwa ajili yetu pia alisulibiwa chini ya Pontio Pilato, akateseka na akazikwa. (Mt. 27.1-2; Marko 15.24-39, 43-47; Mdo 13.29; Rum. 5.8; Ebr. 2.10; 13.12) Siku ya tatu akafufuka kama yasemavyo Maandiko. (Marko 16.5-7; Luka 24.6-8; Mdo 1.3; Rum 6.9; 10.9; 2 Tim. 2.8) Akapaa mbinguni, na ameketi mkono wa kuume wa Baba. (Marko 16.19; Efe. 1.19-20) Atarudi tena katika utukufu, kuhukumu walio hai na wafu, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho. (Isa. 9.7; M,t. 24.30; Yohana 5.22; Mdo 1.11; 17.31; Rum. 14.9; 2 Kor. 5.10; 2 Tim. 4.1)

Ufu. 4.11 Umestahili wewe Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa. Yohana 1.1 Hapo Mwanzo kulikuwa Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 1 Kor.15.3-5 Kwa maana naliwatolea ninyi hapo Mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo Maandiko; na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo Maandiko; na ya kuwa alimtokea Kefa; tena na wale thenashara; Rum. 8.11 Lakini ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu. 1 Pet. 2.9 Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu. 1 The. 4.16-17 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele

Tuna amini katika Roho Mtakatifu, aliye Bwana na Mpaji wa uzima,

(Mwa. 1.1-2; Ayu 33.4; Zab. 104.30; 139.7-8; Luka 4.18-19; Yohana 3.5-6; 1.1-2; 1 Kor. 2.11; Ufu. 3.22) Ambaye anatoka kwa Baba na kwa Mwana, (Yohana 14.16-18, 26; 15.26; 20.22) Ambaye pamoja na Baba, na Mwana, anaabudiwa na kutukuzwa. (Isa. 6.3; Mt. 28.19; 2 Kor. 13.14; Ufu. 4.8) Ambaye alinena kupitia manabii. (Hes. 11.29; Mik. 3.8; Mdo 2.17-18; 2 Pet. 1.21)

Tunaamini katika Kanisa moja takatifu, Katoliki na la Kitume. (Mt. 16.18; Efe. 5.25-28; 1 Kor. 1.2; 10.17; 1 Tim. 3.15; Ufu. 7.9)

Tunatambua ubatizo mmoja kwa ajili ya msamaha wa dhambi, (Mdo 22.16; 1 Pet. 3.21; Efe. 4.4-5) Na tunatazamia kufufuliwa kwa wafu na maisha ya wakati ujao (Isa. 11.6-10; Mik. 4.1-7; Luka 18.29-30; Ufu. 21.1-5; 21.22-22.5) .

Amina.

Made with FlippingBook - Online magazine maker