Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook
2 3 8 /
M U N G U M W A N A
Kiini na Chimbuko: Ukristo Ni Yesu Kristo (muendelezo)
Baba alimtoa Mwana wake mwenyewe kuwa dhabihu ili kuukomboa ulimwengu, ili kufanyika daraja la upatanisho la pengo kati yetu na Mungu kwa sababu ya kutomtii, na kutupa sisi kuzaliwa upya kama watoto wa kuasiliwa katika familia ya Mungu. Mwanamume mmoja alikuwa na jukumu la kuinua daraja la kuinuliwa ili kuruhusu meli zipite kwenye mto ulio chini na kulishusha tena ili treni zivuke nchi kavu. Siku moja, mtoto wa mwanaume huyu alimtembelea, akitaka kumtazama baba yake kazini. Akiwa na shauku kubwa ya kutaka kujua, kama walivyo wavulana wengi, alichungulia kwenye mlango wa dari ambao kila mara uliachwa wazi ili baba yake aweze kutazama mashine kubwa iliyoinua na kushusha daraja. Ghafla, mvulana aliteleza na akaanguka kwenye gia. Baba alipojaribu kumnyooshea mkono na kumtoa nje, alisikia filimbi ya treni iliyokuwa ikikaribia. Alijua magari yangejaa watu na isingewezekana kusimamisha treni iendayo kasi, kwa hiyo, daraja lazima lishushwe! Mtanziko wa kutisha ulimkabili; kwani ikiwa angewaokoa watu, mtoto wake angesagwa na meno ya lile gurudumu. Kwa hasira, alijaribu kumnusuru kijana huyo, lakini hakufanikiwa. Hatimaye, baba aliweka mkono wake kwenye nguzo ya kuwashia mashine. Alinyamaza kisha, huku akitokwa na machozi akaivuta. Mashine ile kubwa ilianza kufanya kazi na daraja likabana kwa wakati ili kuokoa treni. Abiria, bila kujua baba amefanya nini, walikuwa wakicheka na kufurahi; hata hivyo, ni kwamba mlinzi wa daraja alichagua kuokoa maisha yao kwa gharama ya mtoto wake. Hakuna mtu na hakuna chochote kinachoweza kufafanua gharama ya bei ambayo Baba alitoa ili kuturudisha kwake kwa njia ya Kristo. Hii inadhihirisha ukuu wa ajabu wa upendo wa Mungu kwa kila mmoja wetu, kwamba alimtoa Mwana wake wa pekee kwa ajili ya ukombozi wetu.
III. Mwisho, Yesu Si Tu Ufunuo Kamili wa Mungu na Ukombozi Uliokamilika, Yeye Pia Ndiye Kielelezo cha Mwisho cha Utawala na Asili Halisi ya Mwanadamu.
A. Yesu ni kielelezo cha Mungu, mtawala wake, kiwango chake cha mwisho cha vile tulivyo na tutakavyokuwa hivi karibuni. Angalia tena Wakolosai 1:18-19 - Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote. 19 Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae.
Made with FlippingBook - Online magazine maker