Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook
/ 2 4 3
M U N G U M W A N A
K I A M B A T I S H O C H A 4 4 Yesu na Maskini Don L. Davis
Tasnifu: Msingi wa huduma ya Yesu ya Ufalme ulikuwa mabadiliko na kufanywa upya kwa wale walio katika hali ya chini ya maisha, maskini. Alionyesha maono yake binafsi ya moyo kwa jinsi alivyozindua huduma yake, alithibitisha huduma yake, alifafanua moyo na kiini cha huduma, akijihusisha moja kwa moja na maskini.
I. Yesu Alizindua Huduma Yake kwa Kuwafikia Maskini.
A. Mahubiri ya uzinduzi huko Nazareti, Luka 4:16-21 Luka 4:16-21 - Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome. 17 Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa, 18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, 19 Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. 20 Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho. 21 Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu.
B. Maana ya uzinduzi huu 1. Lengo la umakini wake: uchaguzi wake wa maandiko 2. Lengo la wito wake: upako wake wa Roho 3. Madhumuni ya upendo wake: a. Habari Njema kwa maskini b. Kufunguliwa kwa wafungwa c. Vipofu kupata kuona tena d. Kuwaacha huru waliosetwa 4. Lengo la huduma yake: Mwaka wa Bwana uliokubaliwa
Made with FlippingBook - Online magazine maker