Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook

2 4 6 /

M U N G U M W A N A

Yesu na Maskini (muendelezo)

ile ya wonyesho, ambayo si halali kwake kuila wala kwa wale wenziwe, ila kwa makuhani peke yao? 5 Wala hamkusoma katika torati, kwamba siku ya sabato makuhani hekaluni huinajisi sabato wasipate hatia? 6 Lakini nawaambieni, kwamba hapa yupo aliye mkuu kuliko hekalu. 7 Lakini kama mngalijua maana yake maneno haya, NATAKA REHEMA, WALA SI SADAKA, msingaliwalaumu wasio na hatia. 8 Kwa maana Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato. 9 Akaondoka huko, akaingia katika sinagogi lao. 10 Na tazama, yumo mtu mwenye mkono umepooza; wakamwuliza, wakisema, Ni halali kuponya watu siku ya sabato? Wapate kumshitaki. 11 Akawaambia, Ni mtu yupi miongoni mwenu mwenye kondoo mmoja, na yule kondoo ametumbukia shimoni siku ya sabato, asiyemshika akamwopoa? 12 Je! Mtu ni bora kuliko kondoo mara ngapi? Basi ni halali kutenda mema siku ya sabato. 1. Wanafunzi wanaokula nafaka siku ya Sabato 2. Mabishano ya Mafarisayo: “ Tazama! Wanafunzi wako wanafanya neno ambalo si halali kulifanya siku ya sabato.” 3. Majibu ya Yesu: “Nataka rehema, wala si sadaka.” a. Rehema kwa maskini na waliosetwa, sio uaminifu wa kiibada b. Huruma kwa waliosetwa, sio nidhamu ya kidini.

C. Huduma kwa maskini ni kipimo cha litmasi cha wokovu wa kweli .

IV. Yesu Anajihusisha na Maskini Bila Kujibakiza.

A. Wale wasioweza kukulipa, Luka 14:11-15 Luka 14:11-14 - Kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa. 12 Akamwambia na yule aliyemwalika, Ufanyapo chakula cha mchana au cha jioni, usiwaite rafiki zako, wala ndugu zako, wala jamaa zako, wala jirani zako wenye mali; wao wasije wakakualika wewe ukapata malipo. 13 Bali ufanyapo karamu waite maskini, vilema, viwete, vipofu, 14 nawe utakuwa heri, kwa kuwa hao hawana cha kukulipa; kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki.

Made with FlippingBook - Online magazine maker