Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook
2 5 0 /
M U N G U M W A N A
Namna ya Kuandika Kazi Yako (muendelezo)
Ukurasa wa “Kazi Zilizonukuliwa” unatakiwa kuwekwa mwishoni mwa kazi yako. Ukurasa huu: • Unaorodhesha kila chanzo ulichonukuu katika chapisho lako. • Unaandikwa katika mfumo wa kialfabeti kwa kuweka jina la mwisho la mwandishi • Unajumuisha tarehe ya uchapishaji na taarifa kuhusu mchapishaji.
Kutengeneza Ukurasa wa Kazi zenye Nukuu
Sheria zifuatazo za mpangilio zinapaswa kufuatwa: 1. Kichwa cha Habari
Kichwa cha habari “Kazi Zilizonukuliwa” kinatakiwa kitumike na kuwekwa katikati katika mstari wa kwanza wa ukurasa baada ya mstari wa mpaka wa upande wa juu. 2. Maudhui Kila marejeo yanatakiwa kuorodhesha: • Jina kamili la mwandishi (likianza na jina la mwisho) • Tarehe ya kuchapishwa • Kichwa cha habari na taarifa yoyote muhimu (toleo Jipya, toleo la pili, kuchapishwa upya) zilizochukuliwa kutoka kwenye jarada au ukurasa wa kichwa cha habari inatakiwa zionyeshwe. • Mji ambao mchapishaji ana makao yake makuu ikifuatiwa na nukta-mbili na jina la mchapishaji 3. Muundo wa Msingi • Kila taarifa inatakiwa itenganishwe kwa nukta. • Mstari wa pili wa marejeo (na mistari mingine yote inayofuata) inakiwa iwe imeingia ndani kidogo. • Vichwa vya habari vya kitabu vinatakiwa kupigiwa mistari (au kuandikwa kwa italiki). • Vichwa vya habari vya machapisho vinatakiwa viwekwe ndani ya fungua na funga semi. Mfano: Fee, Gordon D. 1991. Gospel and Spirit: Issues in New Testament Hermeneutics . Peabody, MA: Hendrickson publishers.
Made with FlippingBook - Online magazine maker