Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook

2 8 /

M U N G U M W A N A

ni uzushi. Mafundisho mawili ya uzushi mkuu wa kihistoria kuhusu uungu wa Kristo ni Ebionism na Arianism , ambayo yote yanapotosha fundisho la Biblia kuhusu Yesu kama Mwana wa Mungu. • Kuelewa, kuthibitisha, na kuadhimisha uungu wa Yesu ni kiini cha ibada na ufuasi wetu unaoendelea. Kukiri kweli kuhusu Yesu kama Mwana wa Mungu kunaendelea kuwa muhimu kwa kila nyanja ya Imani na ushuhuda wetu kwa ulimwengu.

I. Neno ( Logos ) Aliyekuwepo Awali katika Kanuni ya Imani ya Nikea na Maandiko

Muhtasari wa Sehemu ya 2 ya Video

1

A. Umuhimu wa Kanuni ya Imani kwa Kristolojia

Kabla ya huduma ya Yesu, tunaweza kuzungumza tu juu ya tumaini la Kiyahudi lenye sura tofauti-tofauti kuhusu enzi mpya, mara nyingi likihusisha mtu mmoja au zaidi wa kati au mkombozi—masihi, nabii, shujaa aliyeinuliwa, malaika mkuu, au hata Mungu mwenyewe. Karne moja baadaye sura hizi zote na zaidi au zilibadilishwa au zilielekezwa kumlenga mtu mmoja, Yesu Kristo. Ignatius alizungumza juu ya Yesu kwa maneno ya moja kwa moja kama “Mungu wetu, Yesu (ambaye ni) Kristo” (Efe. 18:2 1 ; Rum. 3:3 2 ), na alionyesha jinsi Kristolojia ilivyokuwa kwenye njia sahihi kuelekea matamko ya Kanuni za Imani za mabaraza ya kiekumene. “Yuko tabibu mmoja, ambaye ni mwili na roho, aliyezaliwa japo hakuzaliwa, ambaye ni Mungu ndani ya mwanadamu, uzima wa kweli katika mauti, wa Mariamu na wa Mungu, ambaye kwanza aweza kuumizwa na kisha hawezi kuumizwa, Yesu Kristo Bwana wetu.” (Efe. 7:2) 1 . Katika kipindi cha miaka mia hiyo, madai ya Ukristo yalijitokeza na kuanza kuchukua sura ya uhakika. ~ James G. G. Dunn. “Christology.” Kamusi ya Biblia ya Anchor. D. N. Freedman, mh. (Mhariri wa elektroniki.). Doubleday: New York, 1996.

1 Barua ya Ignatius kwa Waefeso.

2 Barua ya Ignatius kwa Warumi.

B. Lugha ya Kanuni ya Imani kuhusu uwepo wa Yesu kabla

1. “Tunamwamini Bwana Mmoja Yesu Kristo”: Kanuni ya Imani inakiri uaminifu kamili katika Yesu wa Nazareti kama Bwana na Masihi.

Made with FlippingBook - Online magazine maker