Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook

5 0 /

M U N G U M W A N A

wa Mungu, na bila yeye, mbali na yeye hakuna msamaha, rehema, mwelekeo, au neema. Ikiwa umempata Yesu, umempata. Huhitaji kumtafuta mwingine. Mungu na atupe hekima ya kutambua kwamba Maandiko juu ya Masihi na Ufalme ujao yametimizwa ndani ya Yesu wa Nazareti . Marko 1:14-15 - Hata baada ya Yohana kutiwa gerezani, Yesu akaenda Galilaya, akiihubiri Habari Njema ya Mungu, 15 akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili. Baada ya kutamka na/au kuimba Kanuni ya Imani ya Nikea (katika kiambatisho), sali sala ifuatayo: Mwenyezi Mungu uliyetuumba kwa namna ya ajabu kwa mfano wako na hata hivyo kuturejeza kwa njia ya ajabu zaidi kupitia Mwana wako, Yesu Kristo: Utujalie kushiriki maisha yake ya kiungu anaposhiriki ubinadamu wetu; ambaye sasa yu hai na anatawala pamoja nawe katika umoja wa Roho Mtakatifu Mungu mmoja, milele na milele. ~ Kanisa la Jimbo la Afrika Kusini. Kitabu cha Mhudumu cha Kutumika Pamoja na Ekaristi Takatifu na Sala ya Asubuhi na Jioni . Braamfontein: Idara ya Uchapishaji ya Kanisa la Jimbo la Afrika Kusini. uk. 27.

Kanuni ya Imani ya Nikea na maombi

2

Weka kando vitabu na madokezo yako, kusanya mawazo na tafakari zako, na ufanye jaribio la Somo la 1, Yesu, Masihi na Bwana wa Wote: Alikuja .

Jaribio

Fanya mazoezi pamoja na mwanafunzi mwenzako, andika na/au nukuu kwa kutamka andiko la kukumbuka ulilopewa katika kipindi kilichopita: Yohana 1:14-18.

Mazoezi ya kukariri maandiko

Kusanya muhtasari wako wa kazi ya usomaji ya wiki ililopita, yaani, jibu lako lenye maelezo machache kuhusu mambo muhimu uliyoyaona katika vitabu ulivyoelekezwa kusoma, yaani hoja kuu ambazo waandishi walikusudia kuziwasilisha (taz. Fomu ya Ripoti ya Usomaji).

Kazi za kukusanya

Made with FlippingBook - Online magazine maker