Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook
5 2 /
M U N G U M W A N A
Mtazamo huu unazua maswali mazito kuhusu asili ya Kristo, ufuasi wa Kikristo, na uhalali wa sasa na endelevu wa baadhi ya picha na alama za msingi za maisha ya Kikristo: k.m. msalaba, madhabahu, damu, Mwana-Kondoo, n.k. Mtazamo huu wa mafanikio na baraka unatumia kwa nguvu kubwa baadhi ya maandiko yaliyo chaguliwa, ambayo yote yanaelekea kusisitiza upande wa “kuvaa taji ya ushindi” wa uanafunzi wa Kikristo dhidi ya upande wa “unyenyekevu wa kubeba msalaba.” Je, unadhani tunawezaje kujifunza kuelewa tofauti za mikazo, na Yesu kama Mtumishi wetu Atesekaye anatusaidiaje kuelewa kile ambacho mapenzi ya Mungu yanaweza kuwa kwa ajili yetu katika Kanisa leo?
Yesu, Masihi na Bwana wa Wote: Aliishi Sehemu ya 1: Asili ya Kibinadamu ya Kristo
YALIYOMO
2
Mchungaji Dkt. Don L. Davis
Yesu alikuja duniani kama mwanadamu ili kutufunulia sisi wanadamu utukufu wa Baba na kutukomboa kutoka katika dhambi na nguvu za Shetani. Yesu alikuwa mwanadamu kamili, alichukuliwa mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu na kukaa tumboni mwa Bikira Maria hadi alipozaliwa. Mafundisho mawili ya kizushi ya kale yalipinga kufanyika kwa Yesu kuwa mwanadamu: Unestoria (Nestorianism) – ulidai kwamba Kristo alikuwa watu wawili tofauti , na Ueutikia (Eutychianism) – ulidai kwamba Kristo alikuwa na asili moja iliyochanganyika . Mitaguso ya Nikea (325) na Chalcedon (381) ilisuluhisha mkanganyiko huu, ikithibitisha kwamba Yesu alikuwa Mungu kamili na mwanadamu kamili . Mafundisho mengine ya uzushi yaliyotafsiri vibaya maana ya ubinadamuwa Yesu: Docetism ni uzushi ambao ulidai kwamba Yesu hakuwa mwanadamu na Uapolinari (Apollinarianism) ambao ulidai kwamba Yesu hakuwa mwanadamu kamili . Yesu, hata hivyo, ni mwanadamu kamili na anaweza kutuwakilisha kikamilifu mbele za Mungu kama kuhani wetu mkuu, mpatanishi wetu, na kielelezo kipya kwa ajili ya wanadamu waliotukuzwa kama Adamu wetu wa Pili. Lengo letu la sehemu hii, Asili ya Kibinadamu ya Kristo , ni kukuwezesha kuona kwamba: • Kusudi kuu la kuja kwa Yesu duniani lilikuwa ni kutufunulia utukufu wa Mungu Baba katika nafsi yake, na pia kuwakomboa wanadamu kutoka katika adhabu na nguvu za dhambi na Shetani. • Maandiko yanafundisha kwa hakika kwamba Yesu wa Nazareti ni mwanadamu kamili, ambaye alichukuliwa mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu na kuzaliwa na mwanamke, Bikira Maria.
Muhtasari wa Sehemu ya 1
Made with FlippingBook - Online magazine maker