Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook
/ 6 3
M U N G U M W A N A
c. Yesu alikuwa kiumbe changamani, mchanganyiko wa elementi za kibinadamu na za kiungu.
d. Neno liliutwaa mwili tu; lilichukua nafasi ya nafsi ya mwanadamu. Yesu hakuwa na nafsi ya kibinadamu bali nafsi ya kiungu .
e. Matatizo mengi ya fundisho hili: Yesu, kwa tafsiri hii, hana utashi au mapenzi ya kibinadamu. Ubinadamu haujathibitishwa (hili lilikataliwa kama uzushi katika Mtaguso wa Konstantinopoli [381]).
C. Athari za ubinadamu wa Yesu: Yesu ni mwanadamu kamili.
2
1. Huruma: kama kuhani wetu mkuu, anaweza kuelewa mahitaji na mahangaiko yetu (Ebr. 2:14-18).
2. Uwakilishi: kama Adamu wetu wa pili, anatuwakilisha kikamilifu kwa Baba (Rum. 5:12-).
3. Tumaini la kutokufa: kama achukuaye sura yetu halisi, tunajua kwamba miili yetu siku moja itafanana na mwili wake wa utukufu.
a. 1 Wakorintho 15:48-49
b. Warumi 8:29
c. Wafilipi 3:20-21
d. 1 Yohana 3:2
Made with FlippingBook - Online magazine maker