Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook

7 2 /

M U N G U M W A N A

1. Yesu alizindua huduma yake ya hadhara hukoNazareti kwa kuyanukuu maandiko ya Kimasihi ya Agano la Kale kuhusu Mtumishi wa Yehova Atesekaye (Isa. 61:1 na Lk 4:18-19).

2. Kwa tendo hilo Yesu anajihusianisha na Mtumishi wa Bwana wa Agano la Kale (k.m., nabii Isaya).

a. Alikazia fikra mahitaji ya wanyonge na wenye shida, akidokeza kwamba “wagonjwa tu ndio wanaohitaji tabibu,” (Mk 2:14-17).

b. Aliwakemea viongozi wa kidini kwa kushindwa kuwa na rehema na huruma kwa maskini, (Lk 18:9-14)

2

c. Alifanya namna mtu navyowatendea maskini kuwa kipimo cha ubora wa uhusiano wake na Mungu (Mt. 25:31-46).

3. Yesu anatambuliwa na jamii ya Wakristo wa kwanza kuwa Mtumishi wa Bwana (Yoh. 1:41; Mdo 4:27; Mdo 10:38).

4. Yesu anatimiza ushuhuda wa Agano la Kale kuhusu Mtumishi mwaminifu wa Bwana ambaye angehukumu na kuongoza kwa haki juu ya watu wa Mungu (rej. Mt. 12:16-20 na Isa. 42:1-4).

5. Yesu ni Mtumishi wa Yehova ambaye neno lake la kinabii huleta uzima na nguvu kwa wale wanaolisikia (cf. Mt. 11:29-30 na Isa. 50:4).

6. Yesu katika kifo chake alitimiza sifa za Mtumishi wa Kidhabihu wa ajabu wa Isaya 53, ambaye maisha yake duniani na uzoefu wa mateso yake vingetamatika kwa kifo chake badala ya wanadamu wote (Isa. 53:2-6).

Made with FlippingBook - Online magazine maker