Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook
/ 8 5
M U N G U M W A N A
Yesu, Masihi na Bwana wa Wote Alikufa
S O M O L A 3
Karibu katika Jina lenye nguvu la YesuKristo! Baada ya kusoma, kujifunza, kushiriki katika mijadala, na kutendea kazi yaliyomo katika somo hili, utakuwa na uwezo wa: • Kuelezea, kwa kutumia Maandiko na mifano halisi, umuhimu wa kunyenyekezwa kwa Yesu Kristo, yaani, kushuka kwake kutoka katika uungu na utukufu mbinguni kuja duniani na kufa kwa niaba yetu. • Kuonyesha na kutaja mambo muhiumu kuhusiana na kunyenyekezwa kwa Yesu kupitia kuvaa mwili na maisha na huduma yake. • Kuelezea, kwa kutumia Maandiko na sababu zilizo wazi, jinsi kunyenyekezwa huku kwa Yesu kunavyodhihirishwa hasa katika kifo chake. • Kupanua ufahamu kuhusiana na baadhi ya dhana muhimu za kihistoria kuhusu kifo cha Yesu na jinsi kweli hizi zinatuwezesha kuelewa ni kwa kiwango gani kifo cha Bwana wetu kilikuwa baraka kwa wanadamu. • Dhana hizi ni pamoja na mtazamo wa kifo chake kama fidia kwa ajili yetu, kama upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu, kama dhabihu mbadala badala yetu, kama ushindi dhidi ya shetani na kifo chenyewe, na kama upatanisho kati ya Mungu na wanadamu. • Kueleza jinsi Kanuni ya Imani ya Nikea inavyokiri wazi wazi kwamba Bwana wetu Yesu Kristo alikufa na kuzikwa, na jinsi tendo hili lilivyokuwa kilele cha kunyenyekezwa kwa Bwana wetu duniani kunakoanzia na kushuka kwake kutoka mbinguni, akiuacha utukufu wake wa kimbingu aliokuwa nao hapo awali. • Kufafanua nadharia za upatanisho ambazo zimejitokeza katika historia, ikiwa ni pamoja na kifo chake kama: 1) kielelezo cha kiadili, 2) udhihirisho wa upendo wa Mungu, 3) udhihirisho wa haki ya Mungu, 4) ushindi dhidi ya nguvu za uovu na dhambi, na 5) kukidhi heshima ya Mungu. • Kujenga hoja kuhusu ukweli kwamba hakuna nadharia moja ya kihistoria ya upatanisho ambayo peke yake inaweza kuelezea kwa kina utajiri wa maana ya kifo cha Yesu, badala yake kila moja ina viwango vya ukweli ambavyo vinaweza kutusaidia kupata ufahamu wa kina na kuthamini umuhimu wa kifo cha Yesu kwa ajili yetu.
Malengo ya Somo
3
Made with FlippingBook - Online magazine maker