Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook
8 8 /
M U N G U M W A N A
Baada ya kutamka na/au kuimba Kanuni ya Imani ya Nikea (katika kiambatisho), sali sala ifuatayo: Mungu Mtakatifu na wa milele uliyedhihirisha utukufu wa Mwanao alipoinuliwa msalabani: Kubali sifa na shukrani zetu kwa ajili ya uweza wa ushindi wake na utujalie ili kamwe tusiogope kuteswa au kufa pamoja naye; Mfalme wetu aliyesulubiwa aliye hai, na anayetawala milele pamoja nawe na Roho Mtakatifu, Mungu mmoja milele na hata milele. ~ Kanisa la Jimbo la Afrika Kusini. Kitabu cha Mhudumu cha Kutumika Pamoja na Ekaristi Takatifu na Sala ya Asubuhi na Jioni . Braamfontein: Idara ya Uchapishaji ya Kanisa la Jimbo la Afrika Kusini. uk. 47.
Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi
Weka kando vitabu na madokezo yako, kusanya mawazo na tafakari zako, na ufanye jaribio la Somo la 2, Yesu, Masihi na Bwana wa Wote: Aliishi.
Jaribio
Fanya mazoezi pamoja na mwanafunzi mwenzako, andika na/au nukuu kwa kutamka andiko la kukumbuka ulilopewa katika kipindi kilichopita: Waebrania 2:14-17.
Mazoezi ya kukariri maandiko
3
Kusanya muhtasari wako wa kazi ya usomaji ya wiki ililopita, yaani, jibu lako lenye maelezo machache kuhusu mambo muhimu uliyoyaona katika vitabu ulivyoelekezwa kusoma, yaani hoja kuu ambazo waandishi walikusudia kuziwasilisha (taz. Fomu ya Ripoti ya Usomaji).
Kazi za kukusanya
MIFANO YA REJEA
Msalaba mfukoni mwako
Msalaba bila shaka ni mojawapo ya alama zinazoonekana sana za imani ya Kikristo, na ambayo kusema ukweli haieleweki sana. Leo, msalaba unawakilishwa kwa kila njia inayofikiriwa, kuanzia kwenye vishaufu, pete na vipini hadi kwenye vibweta vya mikufu, juu ya vikuku na Tisheti, na kwenye sanaa na usanifu wa kanisa. Ni bidhaa kuu katika nchi za Magharibi na inayodharauliwa katika sehemu nyingi za dunia. Kampuni moja hutengeneza msalaba wa saizi ya sarafu ambayo inafaa kubebwa mfukoni ili kukukumbusha gharama iliyolipwa kwa ajili ya dhambi zetu. Je, una maoni gani kuhusu biashara ya msalaba, na ni jinsi gani shughuli kama hizo zinaweza kutufanya tusijue maana ya kweli ya mateso ya Kristo?
1
Made with FlippingBook - Online magazine maker