Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

/ 1 0 3

M U N G U M W A N A

I. Mtazamo wa kwanza: Kifo cha Yesu kilikuwa kielelezo (Waunitariani).

Muhtasari wa Sehemu ya 2 ya Video

A. Waandishi na hoja za wale wanaoshikilia mtazamo wa kielelezo:

Hatungeweza kujifunza mambo ya Mungu kwa njia nyingine, isipokuwa kwa Bwana wetu, ambaye akiwa Neno, alifanyika mwanadamu. Kwa maana hakuna kiumbe mwingine aliyekuwa na uwezo wa kutufunulia mambo ya Baba. ~ Irenaeus (c. 180, E/W), 1.526. David W. Bercot, ed. A Dictionary of Early Christian Biliefs . Peabody, MA: Henrickson Publishers, 1998. uk. 43.

1. Faustus na Laelius Socinius, wanatheolojia wa karne ya 16, na Waunitariani wa kisasa.

2. Yesu ni kielelezo chetu cha maana ya msingi ya kuwa na upendo kamili kwa Mungu, ambao unahitajika kwa ajili ya wokovu.

3. Andiko kuu la Biblia: 1 Pet. 2:21

3

4. Tunatiwa moyo na utashi binafsi wa Yesu wa upendo na kujidhabihu; kiwango hiki cha upendo anachoonyesha Yesu kinaweza kuonyeshwa na kila mmoja wetu – inawezekana.

B. Hoja dhidi ya mtazamo wa Kielelezo :

1. Unapuuza Maandiko yote yanayozungumzia kifo cha Yesu kama upatanisho, dhabihu, fidia, na kadhalika.

2. Unapuuza ukweli kwamba kifo cha Yesu kinaweza kutafsiriwa kama sadaka ya dhabihu na kama kielelezo cha sisi kufuata, 1 Pet. 2:21-25.

C. Ni ukweli gani tunaoweza kuupata kutokana na mtazamo huu?

1. Yesu alikufa kama kielelezo cha sisi kufuata.

Made with FlippingBook - Share PDF online