Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

1 1 4 /

M U N G U M W A N A

D. Kumbuka onyo la Paulo! Wagalatia 1:6-9 - Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia injili ya namna nyingine. 7 Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza injili ya Kristo. 8 Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe. 9 Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe. » Katika historia ya Kanisa kumekuwa na mitazamo tofauti kuhusiana na kifo cha Yesu msalabani. » Mitazamo mikuu mitano ndiyo ambayo imetawala katika historia ya Kanisa, kila mmoja ukiwa na vipengele mahususi vya ukweli kuhusu maana ya kusulubishwa kwake kwa ajili yetu. » Kifo cha Yesu kinatutolea kielelezo cha kujitoa kwetu kwa Mungu, kinaonyesha upendo wa Mungu kwetu, kinafunua haki kamilifu ya Mungu, kinashinda nguvu za uovu na dhambi, kinatosheleza heshima ya Mungu, na kufanya upatanisho kati ya uumbaji na mwanadamu na Mungu. » Hakuna nadharia au mtazamo unaoweza kuelezea kikamilifu ukuu na baraka ya kifo chake kwa ajili yetu. Maswali yafuatayo yaliandaliwa ili kukusaidia kupitia kile ulichojifunza katika sehemu ya pili ya video. Kitakachokuwa muhimu katika kuyaelewa vyema maarifa haya ni uwezo wako wa kupitia kwa uangalifu na kimahususi nadharia za upatanisho, kuelewa hoja na ushahidi wa kila moja, na kuweza kuzitathmini kulingana na Maandiko. Tumia maswali yaliyopo hapa chini ili kupitia kwa umakini mitazamo mbalimbali, na uutendee haki kila mtazamo kwa kusikiliza misimamo yote na kutafuta kuielewa kabla ya kuikosoa. Jibu kwa uwazi, kwa mafupi, na kwa msingi wa Maandiko. 1. Kifo cha Yesu Kristo ni kielelezo gani kwetu? Kwa nini isingetosha kuona kifo chake kuwa kielelezo tu ? Hitimisho

3

Sehemu ya 2

Maswali kwa wanafunzi na majibu

Made with FlippingBook - Share PDF online