Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

/ 1 1 5

M U N G U M W A N A

2. Elezea hoja na uthibitisho wa mtazamo ya kifo cha Yesu kama udhihirisho wa upendo wa Mungu. Ni matatizo gani yanayoweza kutokea ikiwa tungetafuta kuufanya huu kuwa mtazamo pekee wa kuaminika kuhusiana na kifo cha Yesu? 3. Kifo cha Yesu kinaonyeshaje dhana kuhusu haki na utawala wa Mungu katika ulimwengu huu? Kwa nini mtazamo huu hautoshi kuwa mtazamo pekee wa kuaminika kuhusu kifo cha Yesu? 4. Ni kwa njia gani kifo cha Yesu kinatoa ushindi juu ya nguvu za uovu, za ibilisi, na hata kifo chenyewe? Je, mtazamo huu, kama mingine, unaweza kueleweka kama mtazamo pekee wa kuaminika au hata mtazamo mkuu kuhusu kifo cha Yesu? 5. Elezea mambo makuu katika nadharia ya kuridhika ya upatanisho. Je, mtazamo huu unaweza kutumika kuwa kielezi sahihi zaidi cha maana ya kifo cha Yesu? 6. Kwa nini ni muhimu kupata ukweli kutoka kwa kila mojawapo ya maoni mbalimbali ya upatanisho ili kutusaidia kuelewa maana kamili ya kifo cha Yesu Kristo? Unyenyekevu unapaswa kuchukua nafasi gani katika kutafakari na kutathmini kwetu maoni mbalimbali? 7. Jadili usemi huu: “Hakuna mtazamo mmoja unaofafanua kwa ukamilifu upana na kina cha ufunuo wa kile ambacho Yesu alitimiza pale Kalvari.” Kwa nini ni lazima kila mara tupime nadharia yoyote ya upatanisho katika msingi wa Maandiko ili kuelewa thamani yake kama maelezo ya msalaba? Somo hili linalenga juu ya kunyekezwa kwa Yesu Kristo kupitia Umwilisho na huduma, na katika maana ya kifo cha Yesu Kristo kama inavyohusiana na wokovu na ukombozi wetu. Kwa njia fulani, kweli zinazohusishwa na mada hizi ni nyenzo katika mikono ya Mungu kwa ajili ya Ufalme wake. Nyuzi zote za ufunuo wa Mungu juu yake mwenyewe kama Muumba na Mkombozi zimeungamanishwa na utu wa Yesu wa Nazareti, maisha yake makamilifu na kifo chake msalabani kama fidia mbadala. Wajibu wetu kama viongozi wa Kikristo juu ya mambo haya uko wazi kabisa: hatupaswi tu kuelewa kweli hizi katika mtazamo wa kibiblia na wa kihistoria, lazima pia tuzitafakari na kuziweka katika vitendo katika maisha na huduma zetu. Tunapaswa kufa, kama Yeye, na tunapaswa kuteseka, kama

3

MUUNGANIKO

Muhtasari wa Dhana Muhimu

Made with FlippingBook - Share PDF online