Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

/ 1 1 9

M U N G U M W A N A

Ufufuo, sio mateso!

Ni wazi kwamba Agano Jipya linazingatia asili ya ufufuo kama fundisho kuu la imani ya Kikristo. Wakorintho wa Kwanza sura ya kumi na tano ni Magna Carta (Hati Kuu) ya fundisho la Kikristo: pasipo ufufuo Ukristo ungekuwa ushuhuda wa bure na wa uongo ambao haubadilishi chochote kimwili au kiroho kwa wale waliodanganyika vya kutosha kuukubali. Wengine wamedai kwamba mkazo wetu unapaswa kuwa juu ya ushindi wa ufufuo na ushindi wa kazi ya Bwana wetu, badala ya kifo cha Yesu na udhalilishaji na jeuri inayohusiana nacho. Watu hao wanadai kwamba tukio muhimu zaidi la ushuhuda wa Kikristo ni Pasaka , sio Ijumaa Kuu , na wanadai zaidi kwamba ukereketwa juu ya kifo na jeuri ya Kalvari hausaidii kiroho wala hauna afya kisaikolojia. Ni wazi, hata hivyo, kwamba mitume waliwapa changamoto waamini wa Kanisa la kwanza kuiga mitazamo na mwenendo wao kwa kufuata kielelezo cha mateso ya Kristo na kifo chake (k.m., Flp. 2:5-11; 1 Pet. 2:21 na kuendelea; Gal. 2:20). Hata hivyo, wengi wa wale wanaopinga mkazo juu ya mateso na kifo huelekea kujikita katika kusaka utele, ustawi, afya, na utajiri wa maisha ya Kikristo badala ya ushirika wa mateso yake ili kufananishwa ustawi, afya, na utajiri wa maisha ya Kikristo badala ya ushirika wa mateso yake ili kufananishwa kifo chake (Flp. 3:10). Kuna uhusiano gani kati ya kusisitiza ufufuo wa Bwana wetu na mateso yake katika suala zima la uenezaji wa kweli wa imani ya Kikristo? Kunyenyekezwa kwa Yesu Kristo, tukitumia maneno ya mwanatheolojia Oden, kunahusu kushuka kwake kutoka mbinguni akiuacha utukufu wake wa kiungu, kuja duniani na kufa kwa ajili ya ulimwengu. Unyenyekevu huu uliakisiwa katika kila nyanja ya Umwilisho wa Yesu na maisha yake duniani, tangu kuzaliwa kwake hadi maisha na huduma yake. Kilele cha kushuka na kunyenyekea huku kinadhihirishwa katika mateso na kifo chake pale Kalvari. Kifo chake kinaweza kueleweka kupitia vipengele mbalimbali vinavyotuwezesha kuelewa vizuri zaidi asili ya wokovu wetu ndani yake: kifo chake kilikuwa fidia kwa ajili yetu, upatanisho wa dhambi zetu, dhabihu mbadala badala yetu, ushindi dhidi ya shetani na kifo chenyewe, na upatanisho kati ya Mungu na wanadamu. Kifo cha Yesu kimeeleweka kwa njia mbalimbali katika historia ya Ukristo. Kila moja ya nadharia hizi za upatanisho inalenga katika mwelekeo fulani wa wokovu, na zikichukuliwa kwa pamoja zinatuwezesha kupata ufahamu mpana zaidi na uelewa wa kina wa umuhimu wa kifo cha Yesu kwa ajili yetu. Kifo cha Yesu na maana yake kimetafsiriwa kama 1) kielelezo cha kiadili, 2) udhihirisho wa upendo wa Mungu, 3) udhihirisho wa haki ya Mungu, 4) ushindi dhidi ya nguvu za uovu na dhambi, na 5) kukidhi heshima ya Mungu. Ingawa hakuna nadharia moja kati

3

3

Marejeo ya Tasnifu ya Somo

Made with FlippingBook - Share PDF online