Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

1 2 0 /

M U N G U M W A N A

ya hizo inayoelezea kikamilifu kifo cha Yesu, kila moja ina kweli zinazoweza kuboresha uelewa wetu wa maana na ukweli wake kwa upana mkubwa zaidi.

Ikiwa utapenda kupata ufahamu wa kina zaidi kuhusu baadhi ya maarifa yaliyomo katika somo hili la Yesu, Masihi na Bwana wa Wote: Alikufa , unaweza kujaribu vitabu vifuatavyo: Brown, Raymond E. The Death of the Messiah . New York: Doubleday, 1994. Kiehl, Erich H. The Passion of Our Lord. Grand Rapids: Baker Book House, 1990. Lohse, Eduard. History of the Suffering and Death of Jesus Christ. Philadelphia: Fortress Press, 1967. Stott, John. The Cross of Christ. Downers Grove, IL: InterVarsity, 1986. Unyenyekevu na kifo cha Yesu Kristo ni kitovu cha imani na utendaji wa Kikristo kiasi kwamba sisi kama viongozi lazima tuweze kuhusianisha maarifa na kweli zake na maisha na huduma zetu kila mara. Jinsi unavyoweka kweli hii katika vitendo katika maisha yako mwenyewe kutaamua ufanisi wako katika kuelezea umuhimu wake katika kanisa lako na ushuhuda wako. Suala la namna ambayo Mungu angekutaka ubadilishe au uboreshe mbinu yako ya huduma kulingana na kweli hizi linategemea sana uwezo wako wa kusikia kile ambacho Roho Mtakatifu anakuambia kuhusu mahali ulipo, mahali ilipo huduma yako na uongozi wako wa kichungaji, na mahali walipo washirika wa kanisa lako. Kadhalika inategemea sana ni nini hasa Mungu anakuita kufanya sasa hivi, kuhusu kweli hizi. Panga kutumia wakati mzuri juma hili kutafakari maana ya kifo cha Kristo, na jinsi maisha yako mwenyewe yanavyohitaji kujawa na maarifa haya zaidi na kuimarishwa na kweli zilizomo. Zaidi ya hayo, unapozingatia kazi yako ya huduma katika moduli hii, unaweza kuitumia ili kuiunganisha na kweli kuhusu unyenyekevu na kifo cha Yesu kwa njia ya huduma kwa vitendo na ya moja kwa moja kwa hadhira yako, yaani yeyote utakayemchagua kumshirikisha maarifa ambayo umeyapokea. Zaidi ya yote, ni lazima tutafute kufahamu namna ambavyo Bwana mwenyewe anataka kutumia maarifa haya katika maisha yetu kuhusiana na unyenyekevu na kifo cha Kristo. Utafute uso wa Bwana wiki hii ili kupata maongozi yake, na urudi wiki ijayo tayari kuwashirikisha wanafunzi wengine wa darasa lako kile ulichokipokea kutoka kwa Bwana.

Nyenzo na Bibliografia

Kuhusianisha somo na huduma

3

Made with FlippingBook - Share PDF online