Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

/ 1 2 1

M U N G U M W A N A

Bwana anaposema nawe, ujue atakupa nafasi ya kuomba na kuombewa katika maeneo ya ukuaji ambayo ni hitaji lako leo. Labda kuna baadhi ya mahitaji maalum ambayo Roho Mtakatifu amekufunulia kupitia kujifunza kwako somo hili juu ya kifo cha Yesu. Tafuta mtu wa kushirikiana naye katika maombi ambaye anaweza kuuelewa moyo wako na mzigo ulionao, na kuungana nawe kuinua mahitaji yako mbele za Bwana. Bila shaka, mwalimu wako yuko tayari sana kutembea nawe katika hili, na viongozi wa kanisa lako, hasa mchungaji wako, bila shaka yuko katika nafasi nzuri zaidi kukusaidia kujibu maswali yoyote magumu yanayotokana na kutafakari kwako juu ya somo hili. Kuwa mwazi kwa Mungu na umruhusu akuongoze jinsi anavyotaka. Zingatia hitaji lako la kuruhusu nia ya Kristo kukaa ndani yako, na kifo cha Yesu kiwe halisi zaidi na zaidi katika kila mwelekeo wa tabia na ushuhuda wako katika Kristo.

Ushauri na maombi

MAZOEZI

1 Petro 2:21-24

Kukariri Maandiko

3

Ili kujiandaa kwa ajili ya kipindi, tafadhali tembelea www.tumi.org/books kupata kazi ya usomaji ya wiki ijayo, au muulize Mkufunzi wako.

Kazi za usomaji

Kama kawaida unapaswa kuja na Fomu ya Ripoti ya Usomaji yenye muhtasari wako wa maeneo ya usomaji ya wiki. Pia, ni muhimu uwe umechagua maandiko kwa ajili ya Kazi ya Ufafanuzi wa Maandiko (eksejesia), na ukabidhi mapendekezo yako kuhusiana na Kazi ya Huduma. Katika somohili, tuliangalia kunyenyekezwa kwaYesuKristokwanjia yaUmwilisho na kifo chake. Tulichunguza baadhi ya vipengele muhimu vya kifo chake kwa ajili ya wokovu: kama dhabihu ya fidia, upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu, dhabihu mbadala badala yetu, ushindi juu ya namna Shetani anavyotushikilia kupitia kifo, na upatanisho kati ya Mungu na wanadamu. Kifo cha Yesu kinatoa kielelezo cha kujitoa kwetu kwa Mungu, kinaonyesha upendo wa Mungu kwetu, kinafunua haki kamilifu ya Mungu, kinashinda nguvu za uovu na dhambi, kinatosheleza heshima ya Mungu. Hakuna nadharia au mtazamo unaoweza kuelezea kikamilifu ukuu na baraka ya kifo chake kwa ajili yetu. Katika somo letu linalofuata, tutaangalia kitovu cha Kristolojia na theolojia ya Kikristo, ufufuo wa Yesu, pamoja na kupaa, na kurudi kwake hivi karibuni. Mungu asifiwe kwa ajili ya Mwokozi na Bwana wetu, Yesu, ambaye alikufa na kufufuka ili kuleta wokovu kwa ulimwengu, na atarudi punde kuuthibitisha utawala wa Mungu kati yetu. Amina!

Kazi nyingine

ukurasa 287  6

Kuelekea somo linalofuata

Made with FlippingBook - Share PDF online