Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

/ 1 2 9

M U N G U M W A N A

YALIYOMO

Yesu, Masihi na Bwana wa Wote: Alifufuka na Atarudi Sehemu ya 1: Kufufuka na Kupaa kwa Yesu Kristo

Mchungaji Dkt. Don L. Davis

Vipengele mbalimbali na maana za kuinuliwa kwa Kristo vinaweza kueleweka kwa uwazi kwa msingi wa matukio mawili muhimu ya wokovu: kufufuka na kupaa kwa Kristo. Ufufuo unatumika kama uthibitisho wa Umasihi na uwana wa Yesu, na kupaa kwake kunampa Mwokozi wetu cheo cha hadhi na mamlaka kinachomruhusu kujaza vitu vyote kwa utukufu wake. Tukio la Kristo (yaani, kuwepo kwa Yesu kabla, maisha yake, huduma, kifo, ufufuo, na utukufu wake) linaweza kufikiriwa kwa maana ya mitazamo au mielekeo miwili, mwelekeo wa kushuka (katika unyonge au kunyenyekezwa), na kupanda (kuinuliwa). Kufufuka na kupaa vinahusishwa moja kwa moja na kuinuliwa kwa Kristo na utukufu wake. Malengo yetu katika sehemu hii, Kufufuka na Kupaa kwa Yesu Kristo , ni kukuwezesha kuona kwamba: • Vipengele na maana mbalimbali za kuinuliwa kwa Kristo vinaweza kueleweka kwa uwazi kwa msingi wa matukio mawili muhimu ya wokovu; Kufufuka na Kupaa kwa Yesu Kristo. • Ufufuo unatumika kama uthibitisho wa Umasihi na uwana wa Yesu, na kupaa kwake kunampa Mwokozi wetu cheo cha hadhi na mamlaka kinachomruhusu kujaza vitu vyote kwa utukufu wake. • Tukio la Kristo (yaani, kuwepo kwa Yesu kabla, maisha yake, huduma, kifo, ufufuo, na utukufu wake) linaweza kufikiriwa kwa maana ya mitazamo au mielekeo miwili, mwelekeo wa kushuka (katika unyonge au kunyenyekezwa), na kupanda (kuinuliwa). Kufufuka na kupaa vinahusishwa moja kwa moja na kuinuliwa kwa Kristo na utukufu wake.

Muhtasari wa Sehemu ya 1

ukurasa 294  4

4

Made with FlippingBook - Share PDF online