Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

1 3 0 /

M U N G U M W A N A

Hebu tuanze kwa kukariri sehemu husika ya Kanuni ya Imani inayohusiana na Somo hili la nne: “Siku ya tatu alifufuka kama yasemavyo Maandiko, akapaa mbinguni na ameketi mkono wa kuume wa Baba. Atarudi tena katika utukufu, kuhukumu walio hai na wafu, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho.”

Muhtasari wa Sehemu ya 1 ya Video

I. Ufufuo wa Yesu Kristo

Mungu amemfanya Bwana Yesu Kristo kuwa limbuko kwa kumfufua katika wafu. ~ Klementi wa Roma (c. 96, W), 1.11. David W. Bercot, ed. A Dictionary of Early

A. Umuhimu wa ufufuo wa Yesu katika imani ya Kikristo na utume

1. Ni fundisho kuu katika imani yote ya Kikristo: (rej. 1 Kor. 15:1-20, “kama Kristo hakufufuka”).

Beliefs . Peabody, MA: Hendrickson Publishers, 1998. uk. 558.

a. Kuhubiri kwa Mitume hakuna thamani na imani yetu katika mahubiri hayo ni bure, mst.14.

4

b. Mitume walimwakilisha Mungu vibaya, kwa kuwa walisema uongo kuhusu Mungu kumfufua Kristo katika wafu, jambo ambalo kwa kweli hakulifanya, mst.15.

c. Imani yetu ni bure kabisa, na bado tuko katika dhambi zetu, mst.17.

d. Wale ambao wamekufa wakiwa wamemwamini Kristo (Kiyunani, “ wamelala usingizi ”) kwa kweli wamepotea.

Nakupa shukrani. . . kwamba naweza kuwa na sehemu. . . katika ufufuo wa uzima wa milele, wa nafsi na mwili. ~ Martyrdom of Polycarp (c. 135, E), 1.42. Ibid. uk. 96.

e. Sisi ni watu wa kusikitisha zaidi na wa kuhurumiwa kuliko watu wote kwa sababu ya udanganyifu na upotovu wa tumaini letu, mst.19.

2. Ufufuo ulikuwa ukweli wa kihistoria na msingi wa mahubiri ya Mitume.

Made with FlippingBook - Share PDF online