Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

/ 1 3 3

M U N G U M W A N A

e. Yesu analinganisha ufufuo wake na wakati wa Yona ndani ya samaki mkubwa (Mt. 12:40).

f. Yesu anaeleza mateso na utukufu wake kwa wanafunzi na Mitume baada ya kufufuka kwake.

(1) Luka 24:26 (2) Luka 24:46

g. Ufafanuzi wa Petro wa Zaburi 16 kama unabii wa Biblia wa kufufuka kwa Yesu (Mdo 2:25-32).

C. Asili ya mwili wa ufufuo wa Yesu

Tunakiri imani yetu kwamba [mwili wa Kristo] umeketi mkono wa kuume wa Baba aliye mbinguni. Na tunatangaza zaidi kwamba utakuja tena kutoka hapo katika fahari yote ya utukufu wa Baba. Kwa hiyo, ni vigumu sana kwetu kusema kwamba [mwili wake] uliharibiwa, kama ilivyo vigumu kwetu sisi kusema kwamba ulikuwa wa dhambi. ~ Tertullian (c. 210, W), 3.535. Ibid. uk. 559.

1. Mwili wake ulikuwa mwili halisi, si mzuka wala mzimu.

4

a. Uliweza kuguswa na kushikwa (Yoh. 20:20).

b. Ulikuwa na alama za mateso na kusulubishwa kwake (Yoh. 20:24 29).

c. Alikula chakula na mwili wake ukapokea virutubisho (chakula na vinywaji), Luka 24:41-43.

2. Mwili wake ulikuwa na sifa zilizovuka mipaka ya miili yetu ya sasa ya asili.

a. Yesu alitokea katikati ya Mitume wakiwa ndani na milango imefungwa (Yoh. 20:19).

Made with FlippingBook - Share PDF online