Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
1 3 6 /
M U N G U M W A N A
c. Wafilipi 3:20-21
d. 1 Yohana 3:1-2
II. Kupaa kwa Yesu Kristo
Yesu angali ameketi pale mkono wa kuume wa Baba – akiwa mtu, na bado ni Mungu. Yeye ndiye Adamu wa mwisho; hata hivyo, Yeye pia ni Neno asilia. Yeye ni nyama na damu, lakini mwili wake ni safi kuliko wetu. ~ Tertullian (c. 210, W), 3.535. Ibid. uk. 559.
A. Umuhimu wake katika ibada na utume wa Kikristo
1. Kutimiza ahadi yake ya kurudi kwa Baba (Yoh. 6:62; 14:2, 12; 16:5, 10, 28; 20:17) kama uthibitisho wa Umasihi na cheo chake kama Mwana.
2. Kumimina Roho Mtakatifu juu ya Kanisa kwa ajili ya ibada na ushuhuda (Yohana 16:7 pamoja na Matendo 1:8).
4
3. Kueneza “nyara” za ushindi wake wa kiungu juu ya ibilisi na nguvu za uovu (Efe. 4:8-10).
4. Kuandaa makao (yaani, Yerusalemu Mpya) kwa ajili ya watu wake (Yoh. 14:2-3).
5. Uhakikisho wa uwepo endelevu wa Yesu pamoja na watu wake (Mt. 28:20 rej. Yoh. 16.7-15).
6. Kama ishara ya Kuja kwake Mara ya Pili katika utukufu (Mdo. 1:9 11).
Made with FlippingBook - Share PDF online