Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

/ 1 3 9

M U N G U M W A N A

(3) Waebrania 9:24 (4) 1 Yohana 2:1-2

3. Yesu anatawala vitu vyote sasa kama Masihi na Bwana, na lazima atawale mpaka maadui wote wawekwe chini ya miguu yake wakati wa Ujio wa Pili.

a. Matazamio ya kiunabii ya Mfalme wa Kimasihi (1) Mwanzo 49:10 (2) Zaburi 89:35-37 (3) Danieli 7:13-14 (4) Isaya 9:6-7

b. Yesu mwenyewe ndiye utimilifu wa unabii wa Agano la Kale kuhusu Mfalme ajaye kutoka katika ukoo wa Daudi, (Zab. 45:6-7 cf. Ebr 1:8). (1) Luka 1:31-33 (2) Waebrania 1:1-3 (3) Ufunuo 19:16

4

c. Kwa sasa anatawala kama Bwana kutoka mahali pake palipoinuliwa, mkono wa kuume wa Mungu, akiwatiisha adui zake na kuuthibitisha tena utawala wa Mungu kupitia watu wake, Kanisa.

(1) Warumi 14:7-9 (2) Waefeso 1:20-23

d. Yeye anategemeza vitu vyote, na anatenda kazi kama kichwa na chanzo cha vitu vyote kwa ajili ya mwili wake, Kanisa (Kol. 1:17 18).

Made with FlippingBook - Share PDF online