Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

1 3 8 /

M U N G U M W A N A

e. Waebrania 10:12

Kufuatia ufufuo wake kutoka kaburini na kupaa hadi mbinguni, Kristo aliketi mkono wa kuume wa Baba. Wanatheolojia wanaita tendo hili “kipindi” cha Kristo. Bila shaka, kishazi cha Biblia, “mkono wa kuume wa Mungu,” ni njia ya kibinadamu ya kurejelea utawala na nguvu za Mungu juu ya ulimwengu mzima. Katika tamaduni za Mashariki, mkono wa kuume wa mfalme ulikuwa wadhifa wa heshima na mamlaka. Kwa hiyo Biblia inaposema Kristo yupo mkono wa kuume wa Mungu tunajua, kama Calvin alivyosema, kwamba Kristo “amewekwa katika serikali ya mbingu na dunia” kwa sababu maneno, “Kristo ameketi upande wa Mungu” haimaanishi kwamba Yesu amepumzika kuifanya kazi Yake. Badala yake inazungumzia utawala wa Kristo kama Mfalme akitumia mamlaka yake ya uwezo wa kiungu juu ya kila mtu na kila kitu. ~ Bruce A. Demarest, Jesus Christ: The God-Man . Eugene, AU: Wipf na Stock Publishers, 1978, uk. 125.

f. 1 Petro 3:22

g. Ufunuo 3:21

h. Ufunuo 22:1

C. Maana za kitheolojia za kupaa kwa Yesu Kristo

1. Yesu amepewa nafasi iliyotukuka ya heshima, mamlaka, na sifa mbele za Mungu: Yeye ndiye Kichwa cha vitu vyote, Kichwa cha Kanisa.

a. Kama mwili wa Kristo, Efe. 1:20-23

4

b. Kama jeshi la Mungu, Mt. 28:18-20

c. Kama Bwana wa Mavuno, Mt. 9:35-38

2. Yesu anadumu siku zote katika kutimiza jukumu lake la ukuhani mkuu kama mwombezi wetu.

a. Maombi yake ya ukuhani mkuu, Yohana 17

b. Maombezi yake kwa waamini leo (1) Warumi 8:33-34 (2) Waebrania 7:25

Made with FlippingBook - Share PDF online