Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
/ 1 4 1
M U N G U M W A N A
Hitimisho
» Matukio mawili muhimu ya Yesu Kristo yanaashiria mwanzo wa kuinuliwa na utukufu wake. » Ufufuo wa Yesu unatumika kama uthibitisho wa Umasihi na cheo chake kama Mwana, na kupaa kwake kunamweka Bwana wetu katika nafasi ya utukufu, uwakilishi wa kikuhani, na ufalme. » Yesu lazima sasa atawale mpaka maadui wote wawekwe chini ya miguu yake. Tafadhali chukua muda wa kutosha kujibu maswali haya na mengine yaliyoibuliwa na video. Kama fundisho kuu la imani ya Kikristo, ufufuo unasimama kama maungamo ya msingi kwa waamini. Kama ishara dhahiri ya ufalme na ushindi wa Kristo, kupaa kunaonyesha sifa kamili ya ushindi wa Yesu juu ya ulimwengu, mwili, na shetani. Kagua kwa umakini mafundisho ya Biblia kupitia maswali yaliyopo hapa chini, na ujenge hoja zako za kupinga au kukubali kwa kutumia Maandiko. 1. Kwa mujibu wa Paulo, ufufuo wa Yesu ndilo fundisho kuu katika maungamo ya Kikristo. Katika akili ya Paulo, ni jambo gani mahususi ambalo ni kweli pia ikiwa kwa kweli Yesu hakufufuka katika wafu ? 2. Ufufuo wa Bwana wetu ulithibitishaje utambulisho wake kama Masihi na Bwana? Jibu kwa ufasaha na kimahususi na utoe uthibitisho wa kimaandiko. 3. Kwa mujibu wa lugha ya Kanuni ya Imani ya Nikea, Yesu alifufuka lini hasa, na ni chanzo gani kinachothibitisha ushuhuda huu? 4. Orodhesha baadhi ya uthibitisho mahususi uliojumuishwa katika simulizi za kihistoria za ufufuo katika Injili zinazothibitisha kwamba Yesu alikufa na kufufuka kutoka kaburini. Unaelezeaje baadhi ya tofauti zinazoonekana katika simulizi mbalimbali za Injili kuhusu habari za ufufuo ? 5. Simulizi za Injili zinafafanuaje sifa mbalimbali za mwili wa Yesu wa ufufuo? Kwa nini ni muhimu kuthibitisha kwamba Yesu alifufuka katika mwili na si kama roho tu? Elezea jibu lako.
Sehemu ya 1
Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
ukurasa 295 6
4
Made with FlippingBook - Share PDF online