Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
1 4 2 /
M U N G U M W A N A
6. Kwa nini kupaa ni muhimu kwa ibada yetu, kujitoa kwetu, na ushuhudiaji wetu wa habari za Bwana Yesu? Lugha ya Kanuni ya Imani inalinganaje na fundisho la Biblia kuhusu kipindi cha sasa cha Kristo mbinguni? 7. Nafasi ya Yesu kama kichwa cha Kanisa inahusianaje na kupaa kwake hata kuketishwa mkono wa kuume wa Baba? Kadhalika, jukumu lake la sasa kama Kuhani Mkuu linahusianaje na kupaa kwake? 8. Utawala wa sasa wa Yesu mbinguni unahusianaje na tumaini tulilo nalo kwamba siku moja atatawala juu ya dunia? Kupaa kwa Yesu kulitoaje uthibitisho kwamba kwa hakika Yeye ndiye Mfalme anayekuja kutoka katika ukoo wa Daudi? 9. Ufufuo wa Yesu na kupaa kwake vinatutiaje moyo katika kumwabudu na kumwadhimisha Kristo kama Bwana wa wote?
Yesu, Masihi na Bwana wa Wote: Alifufuka na Atarudi Sehemu ya 2: Kurudi kwa Yesu Kristo na Utawala wake Ujao
Mchungaji Dkt. Don L. Davis
4
Kauli tatu mahususi katika Kanuni ya Imani ya Nikea zinazungumza juu ya kazi ya wakati ujao ya Yesu duniani . Kwanza, Kanuni ya Imani inazungumza kwamba Yesu Kristo atarudi tena katika utukufu, tendo ambalo litakuwa la ajabu kwa maana ya ukuu wa tendo lenyewe na lina umuhimu kwa wakati wa sasa katika maisha na huduma zetu. Kisha, Kanuni ya Imani inathibitisha kwamba atakuja kuhukumu mataifa, kwa maana Baba amemkabidhi Mwana hukumu yote. Hatimaye, Kanuni ya Imani inakiri kwamba atatawala na Ufalme wake hautakuwa na mwisho, atatimiza unabii wa Agano la Kale na kusimika utawala wa Mungu katika mbingu mpya na nchi mpya. Kweli hizi tatu (yaani, kuja kwake katika utukufu, hukumu yake kwa mataifa, na Ufalme wake wa milele) zinabeba maana kubwa katika maisha na huduma zetu leo. Lengo letu katika sehemu hii, Kurudi kwa Yesu Kristo na Utawala Wake Ujao , ni kukuwezesha kuona kwamba: • Kauli tatu mahususi katika Kanuni ya Imani ya Nikea zinazungumza juu ya kazi ya Yesu duniani katika wakati ujao.
Muhtasari wa sehemu ya 2
Made with FlippingBook - Share PDF online