Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

/ 2 3 1

M U N G U M W A N A

K I A M B A T I S H O C H A 4 2 Namuona Mola Wangu Kitabuni Mwandishi hajulikani

Ninampata Bwana wangu katika Biblia, popote niangaliapo, Yeye ndiye mada ya Biblia, kiini na moyo wa Kitabu; Yeye ni Ua la Sharoni, Yeye ndie urembo wa Yungiyungi, Popote ninapofungua Biblia yangu, Bwana wa Kitabu yuko hapo. Yeye, mwanzoni mwa Kitabu, aliipa dunia umbo lake. Yeye ndiye Safina ya makimbilio, inayobeba mapigo makubwa ya dhoruba Kichaka kinachowaka nyikani, Fimbo ya Haruni inayochipuka, Popote ninapotazama katika Biblia, ninamwona Mwana wa Mungu. Kondoo dume juu ya Mlima Moria, Ngazi kutoka duniani hadi mbinguni, Kamba Nyekundu dirishani, na yule Nyoka aliyeinuliwa juu, Mwamba uliopigwa nyikani, Mchungaji mwenye fimbo na gongo. Uso wa Bwana ninaugundua, popote ninapokifungua Kitabu. Yeye ni Mzao wa Mwanamke, Mwokozi aliyezaliwa na Bikira Yeye ni Mwana wa Daudi, ambaye watu walimkataa kwa dharau, Nguo zake za fadhila na uzuri, yaani, staha ya Haruni. Lakini yeye ni kuhani milele, kwa maana ni Melkizedeki. Bwana wa utukufu wa milele Ambaye Yohana, Mtume, alimwona; Nuru ya mji wa dhahabu, Mwana-Kondoo asiye na doa wala waa, Bwana arusi ajaye usiku wa manane, ambaye Wanawali wanamtazamia. Popote ninapofungua Biblia yangu, namuona Bwana wangu katika Kitabu.

[Tafsiri ya Shairi la “I Find my Lord in the Book”]

Made with FlippingBook - Share PDF online